Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

HATUNAYE TENA! Hiyo ndio kauli unayoweza kuielezea baada ya 
kuwepo kwa taarifa za kufariki dunia kwa video queen hot zaidi 
nchini na muigizaji wa filamu Agnes Gerald maarufu kama Agnes Masogange.
Ni ngumu kuamini kama Masogange amefariki dunia lakini huo 
ndio ukweli.Najua itakuchua dakika kadhaa kutafakari kifo cha 
binti huyo mwenye urembo wake na aliyejaaliwa kuwa na mvuto 
kwa mwenye kuona.
Taarifa kuhusu kifo cha Masogange zinaeleza amefariki dunia leo 
Aprili 20 , mwaka huu katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo 
Mwenge Dar es Salaam. Masogange amefariki dunia akiwa bado 
binti mwenye umri mdogo tu hasa kwa kuzingatia amezaliwa 
mwaka 1989.
Hata hivyo haijafahamika sababu za kifo chake zaidi ya kuelezwa tu amefariki baada ya kuugua muda mfupi na kukimbizwa hospitalini hapo ingawa wapo wanaosema kifo chake kimesababishwa na shinikizo la damu.

Aidha Michuzi Blog imeshuhudia Mwili wa Marehemu Agness Masogange ukiondolewa kituo cha Afya cha Dkt Ngoma  na kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jioni hii.
Kifo chake ni pigo kwa Watanzaia walio wengi na hasa mashabiki 
wa muziki wa kizazi kipya kwani pamoja na kufanya shughuli zake 
binafsi lakini alipata umaarufu zaidi baada ya kuanza kutumiwa na 
wasanii maarufu katika nyimbo zao.
Ni hivi karibuni tu Masogange alitikisa vyombo vya habari nchini 
baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumhukumu kwenda 
jela  miaka miwili au kulipa faini ya Sh.milioni 1.5 baada ya kutiwa 
hatiani kwa makosa mawili la kutumia dawa za kulevya aina ya 
heroine na pili kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.
Hata hivyo Masogange katika kipindi chote cha kesi hiyo ya dawa 
za kulevya hakuwahi kukanusha na baada ya kutolewa hukumu 
alilipa faini ya Sh.milioni 1.5 na akatangaza kuwa a furaha ya aina 
yake kwani alikuwa anabanwa na hata alipotaka kusafiri ilikuwa 
lazima apate kibali.
Hatimaye pamoja na Watanzania kumpenda zaidi Muumba wa 
Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo amemuita.
Bwana ametoa na 
Bwana ametwaa.
Kwake sote tutarejea.
Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...