Na Mwamvua Mwinyi, Kisarawe
WATU wanne wanatuhumiwa kuwa majambazi wamefariki dunia baada ya kujibizana risasi na askari polisi ,wakati wakijaribu kufanya tukio la ujambazi katika nyumba ya Juliana Shirinde ambae ni Mhasibu wa kikundi cha vikoba Ushelisheli,wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Aidha jeshi la Polisi mkoani Pwani,limenasa gari ndogo yenye namba za ubalozi ambazo ni namba bandia T 17 CD 220 ambayo ilikuwa inatumiwa na majambazi kufanya uhalifu.

Akitoa taarifa ya tukio hilo la kukamatwa kwa majambazi hao, Kamanda wa Polisi mkoani humo, ( ACP) Jonathan Shanna ,amesema tukio hilo limetokea April 20 mwaka huu saa moja usiku eneo la Kibaoni wilayani hapo.

Amesema majambazi hayo yanasadikiwa yalikuwa matano wakitumia gari hilo, ambapo mmoja wao alishambuliwa kwa risasi lakini alifanikiwa kutoweka.Kamanda Shanna, alimtaka jambazi alietoweka kujisalimisha ndani ya saa 24 .

Ameeleza zipo tetesi zinazodaiwa baadhi ya waganga wa kienyeji ,ama matabibu ambao huchukua jukumu la kuwatibu majambazi waliojeruhiwa, hivyo ametoa salamu kwao kuwa atakaebainika watamkamata na kumchukulia hatua kali za kisheria .

Kamanda wa polisi Mkoani Pwani, ( ACP )Jonathan Shanna akionyesha silaha na vitu mbalimbali, ikiwemo silaha ya kivita inayokaa na risasi 30 kwa wakati mmoja, ambazo walizikamata katika gari walilolitumia majambazi waliofanya tukio la ujambazi wilayani Kisarawe.
 Kamanda wa polisi Mkoani Pwani,( ACP ) Jonathan Shanna akionyesha gari lililotumika kufanya ujambazi Kisarawe likiwa na namba za bandia za kibalozi huku akiwa ameshika  namba halisi zilizokuwa zimewekwa ndani ya gari hiyo.
 Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoani Pwani ambaye pia ni mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumzia  tukio la ujambazi lililotokea Kisarawe na kuwahakikishia wananchi wa Mkoa huo umejipanga kudhibiti wale wasioutakia mema.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...