Na  Mwandishi Maalum
Tanzania na Israel zimekubaliana kwamba ,  mataifa hayo mawili yana mengi ya kujifunza baina  yao hususani katika eneo la utoaji wa haki na usimamiaji wa sheria.
Hayo yamejiri leo ( jumatatu) wakati Mwanasheria  Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, alipokutana na kufanya mazungumzo  na Waziri wa Sheria wa Israel Bi. Ayalet Shaked.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Jengo la   Mikutano la Kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere ( JNICC), viongozi hao walikubaliana kwamba kuna haja na umuhimu wa   Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Israel kukutana kwa lengo la kuainisha maeneo ambayo Ofisi hizo mbili  zinaweza kushirikiana.
“  Nadhani  tuna mengi ya  kujifunza kutoka kwenu na halikadhalika nanyi kuna maeneo ambayo   mnaweza kujifunza kutoka kwetu. Hivyo basi, ninaamini kwamba pale itakapowezekana,  kuna umuhimu wa mimi kukutana na mwenzangu ili tuweze kuangalia maeneo ya kipaumbele ambayo tunaweza kubadilishana uzoefu na kupanua wigo wa ushirikiano  baina ya nchi zetu”, akasema Dk. Kilangi.
Akayataja maeneo ambayo  anaamini Tanzania na Israel  zinaweza kushirikiana ni pamoja na  namna bora ya kuimarisha mifumo ya utoaji  haki na ushauri wa kisheria wenye tija, pamoja na eneo la uwezeshwji ( capacity  building).
Mwanasheria Mkuu , Dk. Kilangi  ambaye alifuatana na Naibu Mwanasheria Mkuu wa  Serikali Bw, Edson Athnas Makallo, aliyatumia mazungumzo  kati yake na Waziri Shaked kuelezea baadhi ya majukumu yake anayoyatekeleza  kama Mshauri Mkuu wa Serikali katika masuala yote yanayohusu sheria pamoja muundo mpya wa Ofisi  ya Mwanasheria Mkuu ambao umehusisha kuanzishwa kwa Wakili Mkuu wa Serikali.

Kwa upande wake,   Waziri wa Sheria wa Israel, ambaye  Tanzania inakuwa nchi yake ya kwanza kutembelea Barani Afrika, pamoja na kukubaliana na wazo la Dk. Kilangi la kuangalia uwezekano wa  Wanasheria Wakuu kukutana katika muda utakaopangwa. Amesema kwamba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Ofisi nyeti na yenye hadhi ya  juu kabisa katika nchi yoyote ile ikiwamo Israel.
Akaongeza kwamba, majukumu anayoyatekeleza Mwanasheria Mkuu wa  Serikali, Dk. Adelardus Kilangi yanashabihiana na anayotekeleza  Mwanasheria Mkuu wa Israel yakiwamo ya kuisimamia serikali katika  masuala yote yanayohusu sheria, kuiwakilisha serikali katika mahakama za juu na mahakama za chini pamoja na kuendesha mashauri  ya jinai hivyo wawili hao wakipata fursa ya kukutana bila shaka watakuwa na mengi ya kujadiliana na kushirikiana.
Waziri wa Sheria wa Israel Ayalet Shaked anaongoza ujumbe wa  wafanyabiashara kutoka Israel ambao upo hapa nchini kukutana na  wafanyabiashara wa Tanzania.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi akiwa katika mazugumzo na  Waziri wa Sheria wa Israel Bi, Aylet Shaked.  Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika  katika  Ukumbi wa Mikutano wa Kimatifa wa Julius Nyerere ( JNICC) jijini Dar es Salaam,   viongozi hao walikubaliana kwamba Tanzania na Israel  zinayo maeneo ambayo  kila nchi inaweza kujifunza kutoka kwa mwenzie hususani katika  eneo la utoaji  haki na  usimamiaji wa sheria na kwamba kuna haja  kupitia kwa  Wanasheria  Wakuu wa Serikali wa nchi hizo mbili  kukutana ili  kujadiliana maeneo ya  kushirikiana.   Waziri wa Sheria wa Israel  yupo nchini akiongoza ujumbe wa wafanyabiashara.
Katika hatua nyingine, Mwanasheria Mkuu wa  Serikali  Dk. Adelardus Kilangi amekutana na kufanya mazugumzo na  Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bw. Said Hassan Said. Katika mazungumzo  yao viongozi hao wamebadilishana mawazo  ya namna  ya kushirikiana  katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku  yanayosimamia   masuala ya sheria na utaoaji  haki. Pichani Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Bw. Said Hassan Said akimkabidhi Dk. Adelardus Kilangi  Katiba ya Zanzibar ( picha na Ofisi ya AG

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...