Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MAMLAKA
ya Usimamizi wa Bandari (TPA) imeadhimisha miaka 13 tangu kuanzishwa
huku ikijivunia mafanikio ya kuongezeka kwa biashara kuanzia mwaka
2011.
Pia mapato yamekuwa yakiendelea kupanda na kuanzia Julai
mwaka 2017 hadi mwaka 2018 shehena iliyokuwa ikiingia ilianza kupanda na
meli zinazoingia kufikia takriban 3000 kwa mwezi.
Hayo yamesemwa
leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TPA wakati akielezea
Wiki ya Mamlaka hiyo iliyoanza jana na kilele chake kufikiwa Jumapili.Ambapo
watatumia maadhimiaho hayo kueleza walikotoka tangu April 2005, walipo
na wanakotarajia kwenda kwa ajili ya kuboresha zaidi huduma kwa
biashara.
Amesema TPA imekuwa ikiendelea kuboresha utoaji wa
huduma na kuongeza masoko huku wakikusanya Sh.bilioni 420 kwa kipindi
cha miezi sita iliyopita."Mamlaka hiyo, inalenga kuboresha zaidi huduma
zake, kwa kuandaa mazingira ya serikali kupata mapato yake kwa kuwa
kati ya asilimia 45 hadi kufikia 55 ya kodi inayokusanywa na Mamlaka ya
Mapato, hupatikana TPA," amesema.
Kakoko amesema wanatarajia
kutekeleza mradi ya ujenzi wa bandari kavu katika baadhi ya mikoa
ikiwemo Kigoma, Arusha, Mbeya na hata Mwanza wanalenga kuwapa unafuu
wateja wao kutoka nje ya nchi wanaokuwa wakifuatilia bidhaa katika
Mamlaka hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Profesa Ignas Rubaratuka akizungumza kuhusiana na maadhimisho ya miaka 13 ya Mamlaka usimamizi wa bandari yaliyoanza leo , jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mhandisi Deosdidit Kakoko akizungumza na waandishi kuhusiana na mafanikio ya kuanzishwa kwa mamlaka ya usimamizi wa bandari, leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Fransisca Muindi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma watazozitoa katika maadhimisho ya miaka 13 ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...