Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe Selemani Jafo (Mb) amepiga marufuku uchimbaji wa mchanga unaoendelea katika mito mbalimbali Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Jafo ametoa katazo hilo wakati wa ziara yake ya kuangalia athari zilizotokana na mafuriko katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala leo 20 Aprili 2018. Akiwa katika kata ya Gongolamboto eneo la Ulongoni A na Ulongoni B, amejionea jinsi ambavyo mafuriko yaliyotokana na wingi wa mvua zilizonyesha yalivyoharibu madaraja na kuacha athari kubwa kwa wananchi. 
“Nimejionea mwenyewe jinsi ambavyo mvua hizi zimeleta athari kubwa hapa na kusababisha mawasiliano kukatika baina yenu nyinyi na wenzenu wa upande wa pili. Lakini niwaambie kuwa kwa sehemu kubwa baadhi ya wananchi wanachangia uharibifu wa maeneo haya kutokana na uchimbaji wa mchanga unaoendelea na kusababisha uharibufu katika kingo za mito pamoja na miundombinu hii iliyojengwa,” alieleza Mhe. Jafo
Waziri ameeleza kuwa miundombinu inajengwa kwa gharama kubwa na Serikali lakini wapo watu ambao wanaiharibu kwa makusudi kutokana na uchimbaji wa mchanga, hivyo akaeleza kuwa Serikali haitavumilia swala hilo.“Hatuwezi kuzizuia mvua zisinyeshe lakini hatuwezi kuvumilia kuwaacha watu wanaoharibu miundombinu na kingo za mto kwa kuchimba mchanga. Hivyo kuanzia leo napiga marufuku uchimbaji wa mchanga katika maeneo yote ya mito ya Dar es Salaam,” ameagiza Waziri Jafo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema wakionyeshana  maeneo ya daraja yalivyo haribika na mafuriko.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na viongozi wengine katika ukaguzi wa athari za mvua.
 Maeneo yaliyoharibiwa na Mvua
 Maeneo yaliyoharibiwa na mvua

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...