Na Richard Mwaikenda, Kivule, Dar

Viongozi wa Kata ya Kivule, Ukonga Dar, wameunganisha nguvu kuwasaka vibaka wanaowapora watu wanaopita wakati wa usiku katika Daraja linalojengwa MTO Kizinga. 

Uamuzi huo umefanywa baada hivi karibuni Majira ya SAA 5 usiku ambapo mtu mmoja aliyekuwa akivuka katika Daraja la muda kuporwa na vibaka Simu na vitu vingine. 

Tukio hili aliliripoti kituo kidogo cha POLISI cha Kitunda, na kwa viongozi wa Kata ya Kivule, akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kivule, Amos Angaya na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kerezange, Ismail Ibrahim. 

Mwandishi wa Habari hii alishuhudia viongozi hao wakiwa wamemuweka chini ya ulinzi, Kijana Jaffari aliyekamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika uporaji huo akishirikiana na wenzie.Viongozi hao walimnasa 'Kibaka' huyo kwa ushirikiano Mkubwa na waendesha bodaboda pamoja na wafanyabiashara ndogondogo wanaoendesha shughuli zao darajani hapo. 

Walimnasa Jaffari baada ya kutumia mbinu ya kuwatishia wanaoendesha shughuli zao darajani hapo kwamba wasipowataja vibaka basi wote watafukuzwa eneo hilo.Walimnasa Jaffari baada ya kutumia mbinu ya kuwatishia wanaoendesha shughuli zao darajani hapo kwamba wasipowataja vibaka basi wote watafukuzwa eneo hilo. 

Kwa umoja wao, viongozi hao waliapa kutokomeza vitendo vya uovu vilivyoanza kuota mizizi katika eneo hilo la Daraja ambalo limekata mawasiliano ya usafiri Kati ya Kivule Mwembeni na Silari baada Daraja bovu kuvunjwa na kuanza kujenga jipya.Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kerezange, Ismail Ibrahim, Ujenzi wa Daraja hilo unatarajiwa kukamilika Mei, Mwaka huu. 

Hivi sasa daladala kutoka Banana zinaishia upande wa Mwembeni na zinazotoka Frem kumi zinaishia Silari. Magari mengine yanapitia Daraja la Bombambili. 
Daraja la Kivule likiendelea kujengwa katika Mto Kizinga eneo la Sirali,Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wakipita kwenye daraja la muda baada lile la awali kubomolewa kupisha ujenzi wa daraja hilo jipya ambalo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi ujao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...