BAADHI ya Waganga wa Tiba asili mkoani Njombe wameiomba Serikali ya mkoa huo kuchukua hatua kali dhidi ya watu ambao wanajifanya waganga nakwenda kufanya utapeli kwa waganga kinyume cha Sheria ya Tiba asili na mbadala Na 23 ya 2002.

Wamesema kuwa kwa muda mrefu katika mkoa pamekuwepo na watu ambao wanajifanya waganga wa tiba asili na kupita kwa waganga kufanya utapeli kwa kisingio kuwa waganga hao wanafanya kazi wakiwa hawana vyeti vya baraza la tiba asili au vyama husika.

Akizungumzia hali Mmoja wa waganga wa tiba asili mkoani humo ambapo pia ni Katibu wa Chama cha Baraza la waganga Tanzania Geofredi  Mgwila alisema Kweli watu hao wamewatapeli mno waganga.

Amesema kuwa yeye kama kiongozi wa Chama amefurahishwa na maamuzi ya viongozi kutoka Ofisi ya mganga mkuu wa wilaya chini ya Mratibu wake kwa kuliona tatizo hilo nakuaza kuchukua hatua.

"Nikweli waganga wamelia kwa muda mwingi na kulikuwa hakuna kinachoendelea lakini baada vuguvugu hili kujitokeza viongozi husika kwa maana wenye dhamana wameujuwa ukweli na wameaza kuchukua hatua. "amesema mgwila

Waganga hao wamesema kuna wezao ambao wamejiviga Joho la uganga lakini kihalisia hawana taaluma hiyo walikuwa wanapita kwa wagana nakuwatapeli fedha nyingi wengine walitapeliwa hadi kiasi cha shilingi laki 300,000 hadi milioni 1000,000.

Kwaupande wake mkuu wa wilaya ya Halmashauri ya Njombe Mji Luncy Msafiri akizungumzia utapeli huo amesema waganga hao wanatakiwa watoe taarifa kwa viongozi wao ikiwa pamoja na yeye.

Pia amesema kuwa wakiona kuna watu wanakuja kwenye maeneo yao lazima watoe taarifa kwa viongozi wao wa vijiji akiwepo mtendaji.nakudai hata kama wangekuwa polisi lazima pawepo na viongozi husika.

Naye Mwenyekiti  Baraza la tiba asili Taifa Edmund Kayombo awali akizungumzia uwepo wa matapeli hao amesema wanapaswa kukamatwa kwani wanachokifanya ni ulaghai.

Amesema kuwa Chama ambacho anakitambua katika mkoa huo ni kimoja tu ambacho ni Baraza la Waganga wa Tiba Asili Tanzania BAWATA hivyo kama kuna wengine hao yeye hawajuwi .

"Ndugu mwandishi kwasababu uko huko naomba utusaidie kwa kuuliza hata usajili wao pamoja na vyeti vyao nasisi tutatuma wasaidizi wetu kufuatilia jambo hili. "Amesema Kayombo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...