Na: Geofrey Tengeneza-Capetown Afrika Kusini

Banda la Tanzania katika maonesho ya Kimataifa ya WTM Afrika yanayofanyika jijini Capetown Afrika Kusini limeendelea kutembelewa na watu wengi wanaotembelea maonesho haya kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali zinazohusu Tanzania na vivutio vyake vya utalii sambamba na kufanyamzungumzo ya kibiashara na wafanyabiashara katika sekta ya utalii kutoka Tanzania.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi umebaini kuwa watu wengi wanaotembelea banda la Tanzania wamekuwa wakivutiwa zaidi na yanayotolewa kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo nchini kama vile mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, pori la akiba la Selous n.k

Kwa upande wa wadau wa utalii kutoka sekta binafsi kutoka Tanzania wanaoshiriki maonesho haya wameelezea kuridhishwa kwao na namna wanavyoendelea kukutana na kuingia makubaliano na wafanyabiashara wenzao wa utalii wakubwa wa kimataifa.

“ Namshukuru Mungu maonesho ni mazuri na nimefanikiwa kukutana na wafanyabiashara ya utalii kutoka mataifa mbalimbali na kufanya makubaliano katika biashara yetu hii” anasema Bw. Naiman Meyassy Mkurugenzi wa kampuni ya usafirishaji watalii ya Quest Horizonya jijini Arusha.

Mapema Naibu balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Bi Rosemary Jairo alitembelea banda la Tanzania na kuelezea kufurahishwa kwake namna ilivyojipanga na kushiriki vema katika onesho hili. “Nimefurahishwa sana na banda letu na namna mnavyoitangaza nchi yetu, napenda niwaponze sana Bodi ya Utalii kwa uratibu mzuri wa ushiriki wetu kama nchi” alisema naibu Balozi.

Katika onesho hili la WTM Afrika mwaka huu Tanzania inawakilishwa na makampuni 17 kutoka sekta binafi chini ya uratibu wa Bodi ya utalii Tanzania (TTB) wanaoshiriki katika banda la Tanzania wakati makampuni mengine zaidi ya 10 yanashiriki binafsi yakiwa na mabanda yao katika maonesho hayo. Mbali tna TTB taasisi nyingine zinazoshiriki maonesho hayo ni Shirika la Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya hifadhi ya Bonde la Ngorongoro na Kamisheni ya utalii Zanzibar.

Meneja Utafiti na Maendeleowa Bodi ya Utalii Tanzania, Ndugu Gladstone Mlay akitoamaelezo kwa wageni waliyotembelea banda la Tanzania katika maonesho ya utalii “World Travel Market (WTM)” yanayofanyika nchini Afrika Kusini. 
Baadhi ya mawakala wa utalii wa Tanzania waliyoshirikikatika maonesho ya Utalii ya WTM Afrika 2018 wakiuza huduma za utalii wanazozitoa kwa wageni waliyotembelea Banda la Tanzania. 
Baadhi ya mawakala wa utalii wa Tanzania waliyoshirikikatika maonesho ya Utalii ya WTM Afrika 2018 wakiuza huduma za utalii wanazozitoa kwa wageni waliyotembelea Banda la Tanzania. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...