Waziri Wa mambo ya ndani Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amewasihi viongozi mbalimbali wa dini nchini wakiwemo Maaskofu na Mashekh kutumia muda wao mwingi kwa kutembelea mikoa mbalimbali nchini kunapotokea zaidi matukio ya kikatili ikiwemo mauaji ili kuhubiri injili wananchi wawe na hofu na Mungu jambo litakalopelekea kupunguza ukatili na watu kumjua Mungu. 

Dkt Nchemba ameyasema hayo Wakati akimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu alipokuwa akihutubia mamia ya waumini kwenye Tamasha La muziki Wa Injili lililoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ambayo huratibu matamasha hayo kila mwaka. 

Dkt Mwigulu aliwasihi wananchi kwa mshikamano na wingi wao Kuendelea kumuombea Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwani anafanya kazi kubwa katika kuwatumikia watanzania ikiwa ni pamoja na usimamizi mzuri Wa Rasilimali za Taifa ambazo amekusudia kuwanufaisha watanzania wote kupitia uchumi fungamanishi. 

Alisema nia na Dira ya Rais Magufuli ni msisitizo mkubwa Wa umuhimu Wa maslahi kwa watanzania huku akiwasihi maaskofu Wa makanisa yote nchini kuendelea kueneza neno la Mungu kwani matukio yanayotokea ya mauaji yanasababishwa na wananchi kutomjua Mungu kwa kufanya imani za kishirikiana na ukatili kwa watoto, ubakaji wa wanawake, ulawiti, unyanyasaji wa wazee na wananchi wengi kwa ujumla wake. 

Katika tamasha hilo Dkt Mwigulu pia Amezindua albamu ya Msanii nguli Wa nyimbo za injili nchini Tanzania Bi Rose Muhando ijulikanayo kama USIVUNJIKE MOYO na kununua albamu hiyo kwa Shilingi 500,000 huku tamasha hilo likichagizwa na waimbaji 17 Wa ndani na nje ya nchi. 
 Mgeni Rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba na Alex Msama Mkurugenzi wa Msama Promotion wakizindua albam ya mwimbaji Rose Muhando inayojulikana kwa jina la “Usife Moyo” kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika jana jioni kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo waimbaji mbalimbali wa injili wameshiriki katika tamasha hilo.

Mwimbaji Rose Muhando amefanya mambo makubwa wakati alipotumbuiza moja ya kibao chake kipya cha "Lazima Wakae" kilichomo katika albam yake hiyo ambapo mashabiki walishindwa kukaa jukwaani na kucheza wakati wote alipokuwa akitumbuiza.

Baadhi ya waimbaji walioshiriki katika tamasha hilo leo kwenye tamasha hilo ni, Upendo Nkone, Christina Shusho, Beatrice Mwaipaja, Martha Baraka,  Joshua Mlelwa, ,Paul Clement, Sifaeli Mwabuka Dan M kutoka Kenya, Christopher Mwahangila,Bonny Mwaiteje, na wengine wengi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akionesha albam ya "Usife Moyo" ya Rose Muhando,  kulia ni  Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama na Kushoto ni Rose Muhando wakishiriki tukio hilo katika Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana jioni
 Dk Mwigulu akimpongeza Rose Muhando mara baada ya kuizindua albamu yake iliyosheni nyimbo kazi nzuri alioifanya ya utunzi wa nyimbo zenye kuielimisha jamii katika nyanja.
Mwimbaji nyota wa nyimbo za Injili Rose Muhanda akiimba moja ya wimbo wake mpya uliomo kwenye albamu yake mpya  ya 'Usife Moyo' uitwao 'lazima wakae 'mbele ya umati wa wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi,ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Mwigulu Nchemba.
 Waziri wa Mambo ya Ndani,Dkt Mwigulu Nchemba akipokelewa na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mh.John Mongela mara baada ya kuwasili uwanja wa CCM Kirumba,tayari kwa kuzindua tamasha la pasaka kwa mara ya kwanza chini ya Kampuni ya Msama Promotions Ltd sambamba na uzinduzi wa albamu ya Muimbaji nyota wa muziki wa Injili Rose Muhanda iitwaya 'Usife Moyo' yenye jumla ya nyimbo saba. 
 Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika tamasha la pasaka mapema jana jioni ndani ya uwanja wa CCM 
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambae pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula akimtunza muimbaji wa nyimbo za injili Christopher Mwahangila mapema jana jioni ndani ya tamasha la pasaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...