CHINA imetaka watanzania kutumia fursa ya kuwa na maji mengi na ardhi ya kutosha kufanya shughuli za kilimo na kuzalisha mazao mengi ambayo wanaweza kuyauza nchini humo na pia kuyatumia kama malighafi kwa viwanda vya ndani.

Taifa hilo kubwa kiuchumi duniani, limesema kwamba ufunguo wa maendeleo ya viwanda upo katika kilimo na biashara ya kilimo hivyo ipo haja kwa watanzania kufanya bidii katika kufanikisha kilimo.Kauli hiyo imetolewa na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke kwenye mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk Reginald Mengi, ofisini kwa mwenyekiti huyo mwishoni mwa wiki.

Katika mazungumzo hayo Dk Mengi aligusia zaidi kuhusu China kuona haja ya kusaidia kuinua kilimo cha Tanzania kutokana na mabadiliko yanayofanywa Tanzania ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda.Alisema uchumi huo utawezekana kwa kutumia rasilimali za kilimo kama malighafi na kilimo cha Tanzania kinahitaji sapoti kubwa ya kukifanya kuwa cha biashara.

Balozi wa China alikiri kwamba ipo haja ya kukibadili kilimo cha Tanzania ambacho kwa sasa ni cha kifamilia zaidi na kuwa cha biashara na kusema wapo tayari kushiriki katika ndoto za watanzania kwenda kwenye uchumi wa viwanda kwa kutegemea malighafi za kilimo.Hata hivyo alisema kwamba China inahitaji sana mazao ya kilimo kutoka Tanzania, kasoro ni kuwa uzalishaji bado ni mdogo sana.

Alitolea mfano wa kuwepo kwa kiwanda cha mafuta ya kula ya alizeti kwamba mbegu huwa hazitoshi na hivyo kiwanda hicho cha Wachina kulazimika kuagiza mbegu kutoka nje.Alisema kwa sasa kiwanda hicho kinatengeneza tani elfu 10 za mafuta wakati uwezo wa kiwanda ni tani laki moja kwa mwaka.
Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. Wang Ke (kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi kuhusu ushirikiano wa kibiashara baina ya makampuni ya China na Tanzania ofisini kwa mwenyekiti huyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. Wang Ke (kushoto) wakati wa mazungumzo kuhusu ushirikiano wa kibiashara baina ya makampuni ya China na Tanzania ofisini kwa mwenyekiti huyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. Wang Ke akisoma muonekano wa mbele wa kitabu kinachozungumzia maisha ya Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi ulioandikwa “I Can, I Must, I Will - The Spirit of Success” wakati wa mazungumzo yao kuhusu ushirikiano wa kibiashara baina ya makampuni ya China na Tanzania ofisini kwa mwenyekiti huyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. Wang Ke akimkabidhi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi zawadi ya kasha la majani ya chai (China Green Tea) kutoka nchini China mara baada ya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa kibiashara baina ya makampuni ya China na Tanzania ofisini kwa mwenyekiti huyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...