Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
BALOZI wa India nchini Tanzania Sandeep Arya amewahimiza
Watanzania kuchangia fursa za elimu ya juu inayotolewa katika
nchi yao huku akifafanua mkakati walio nao ni kutoa elimu kwa
wanafunzi 200,000 kutoka nje ya nchi na kuwasaidia kupata elimu
bora na ufanisi kutoka vyuo mbalimbali nchini humo.
Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza
fursa za kielimu zinazopatikana nchini India ambapo hafla hiyo
ilihudhuriwa pia na viongozi wa Serikali, shule, vyuo na taasisi ya
elimu ya juu.
Hivyo, amesema anawaalika watanzania kwenda kusoma nchini
India ili kupata uzoefu na kukutana na wanafunzi kutoka nchi
nyingine katika elimu ya juu katika vyuo vya nchini humo na
kuongeza Tanzania na India wana urafiki wa muda mrefu na hiyo
imesaidia Watanzania wengi kusoma nchini India .
"Kuna watanzania wengi ambao wamesoma kwenye vyuo
vilivyopo nchini India na mchango wao katika maendeleo ya nchi
ni mkubwa.Hivyo tunaendelea kuwakarabisha kwa wanaotoaka
kusoma masomo ya elimu ya juu kusoma India , tunajivunia elimu
bora ambayo inatolewa na yenye tija ya kuleta
maendeleo,"amesema Balozi Arya.
Aidha amesema wanaotaka kwenda kusoma India wanaweza
kupata taarifa kupitia tovuti ya www.studyinindia.gov.in portal.
Amefafanua kuwa elimu wanayoitoa ipo katika uhalisia katika
masuala ya elimu, uchumi na jamii kwa ujumla na hivyo
watanzania kusoma nchini India ni fursa ya kubadilisha sekta
mbalimbali kutokana na elimu watakayoipata.
Kwa upande wake Mhitimu wa Symbiosis International (Deemed
University)India Angelelda William amewahimiza vijana wa
kitanzania kwenda kusoma kwenye chuo ambacho yeye amesoma
kutokana na ubora wa elimu inayotolewa chuoni hapo.
Amesema kwa atakayekwenda kusoma chuoni hapo hatajua ada
ambayo anaitoa huku akisisitiza baada ya kuhitimu katika chuo
hicho uwezo wake katika kufanya mambo ni mkubwa.
Kuhusu elimu inayotolewa nchini India amesema vyuo vingi vya
nchini hiyo vimejikita kutoa elimu ya vitendo zaidi badala ya
kuandika na sababu kubwa ni wanamuandaa mwanafunzi
kufanya kazi kwa vitendo zaidi badala ya kuandika kwenye
makaratasi.
”Nimesoma katika Chuo cha Symbiosis ambacho kimejikita kutoa
elimu yenye ubora wa hali ya juu.Nitumie nafasi hii kuwaomba
vijana wenzangu wanapofikia kwenda kusoma India basi chaguo
lao la kwanza liwe kwenye chuo hiki maana nimekaa na nakijua
vizuri,"amesema William.
Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu ubora wa elimu ya juu unaotolewa na vyuo vya nchini India.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa elimu wakimsikiliza Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya wakati anazungumzia elimu ya juu inayotolewa nchini India
Mhitimu wa Symbiosis International (Deemed)Univesity Angelelda Willim(kushoto) akiwa na Ofisa wa Ofa za Kimataifa na Mahusiano ya Wanafunzi wa Symbiosis(kulia)wakitoa maelezo kuhusu ubora wa chuo chao leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa Kituo cha Chanel Ten jijini Dar es Salaam Fred Mwanjala na Beatrice Erick wakipata maelezo kuhusu namna ya kujiunga na moja ya chuo cha nchini India.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...