Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (kushoto) akizungumza na
baadhi ya maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini, juu ya
kuangalia njia bora za kudumisha uhusiano baina ya Benki ya CRDB na
Jeshi la Magereza nchini, katika Makao Makuu wa Magereza, jijini Dar es
salaam, Mei 23, 2018. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza
nchini, Dkt. Juma Malewa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB Dokta Charles Kimei leo amekutana na Mkuu wa
Jeshi la Magereza nchini Dokta Juma Malewa ili kuangalia njia bora zaidi
za kudumisha na kuboresha uhusiano baina ya pande zote mbili.
Akizungumza katika mkutano huo ambao pia ulijumuisha maafisa waandamizi
kutoka Benki ya CRDB na Jeshi la Magereza, Dokta Kimei alilishukuru
Jeshi hilo kwa kuwa mdau mkubwa wa Benki kupitia mikopo, akaunti za
mishahara za askari na SACCOSS ya Magereza ambayo kwa muda mrefu imekuwa
ikitoa huduma kwa askari Magereza.
“Nichukue fursa hii kulishukuru Jeshi la Magereza kwa biashara ambayo limekuwa likitupatia, niipongeze SACCOSS ya Magereza kwa uamuzi wa kuwa Wakala wa FahariHuduma, hii si tu itawaongezea kipato kupitia kamisheni za uwakala, pia itasogeza huduma za kibenki karibu na Maaskari Magereza”, alisema Dokta Kimei.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akizungumza katika kikao na uongozi wa Benki ya CRDB, uliomtembelea ofinisi kwake, Makao Makuu ya Magereza jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei.
Akielezea juu ya fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB kwa wafanyakazi Dokta Kimei alisema hivi karibuni Benki imeshusha riba inayo toza katika mikopo binafsi toka 20% mpaka 17%, muda wa marejesho umeongezwa toka miezi 72 hadi miezi 84, wakati kiwango cha kukopa kimeongezwa kutoka shilingi milioni 50 mpaka kufikia Shilingi Milioni 100 hivyo kuwapa wateja wigo mpana zaidi wa kukopa ili kufikia malengo.
Dokta
Kimei pia alitumia fursa hiyo kuwahamasisha askari wa Jeshi la Magereza
kuchangamkia fursa hiyo ya mikopnnno huku akibainisha ya kuwa Benki ya
CRDB imeanzisha utaratibu maalum wa kununua madeni na mikopo ya askari
kutoka katika Taasisi zingine za Kifedha. Hivyo kutoa fursa kwa askari
wenye mikopo Benki nyingine, kukopa toka Benki yao pendwa ya CRDB.
Mpaka kufikia mwisho wa mwezi Aprili 2018 tayari Benki ya CRDB ilikuwa
imeshakopesha zaidi ya maofisa 5,415 wa Jeshi la Magereza ambapo jumla
ya shilingi 29.4 bilioni zilikuwa zimekopeshwa kwao.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (kushoto) akimkabidhi zawadi maalum, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa, wakati alipomtembelea ofisini kwake, Makao Makuu wa Magereza, jijini Dar es salaam, Mei 23, 2018. Mkutano huo ulikuwa na lengo kudumisha uhusiano wa kibiashara baina ya Benki ya CRDB na Jeshi la Magereza nchini.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Dokta Juma Malewa alimshukuru Dokta Kimei kwa kutembelea Jeshi hilo na kuipongeza Benki ya CRDB kwa maboresho hayo katika huduma zake, huku akiisifu zaidi huduma ya Salary Advance ambayo alisema kwa kiasi kikubwa imesaidia kuboresha maisha ya askari. Dokta Malewa alisema katika maboresho hayo yanayoendelea Jeshi la Magereza lingependa kutumia mfumo wa kibenki katika kukusanya mapato yake katika miradi na huduma mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.
“Nikuombe Dokta Kimei na uongozi mzima wa Benki ya CRDB kuona uwezekano wa kuweka huduma za kibenki kama ATM na Matawi kwenye maeneo ya Magereza yenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo”, aliongezea Dokta Malewa. Dokta Malewa pia aliiomba Benki ya CRDB kushiriki katika miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa na Jeshi hilo ikiwamo ujenzi wa hospitali ya Jeshi la Magereza Ukonga, miradi ya Kilimo cha kisasa na chenye tija, mradi wa kokoto Msalato pamoja na uwekezaji katika miradi ya viwanda vidogo vidogo.
Dokta Kimei alimhakikishia Mkuu wa Jeshi la Magereza kuwa Benki ya CRDB ipo tayari kushirikiana na Jeshi hilo katika miradi mbalimbali ambayo wamepanga kuitekeleza, huku akihaahidi kutuma timu ya wataalam kutoka Benki ya CRDB kufanya upembuzi yakinifu juu ya kuweka ATM na kufungua vito vya kutolea huduma katika maeneo ya Jeshi la Magereza ilikufikisha huduma kwa akari kwa urahisi.
“Matarajio
yangu ni kuona uhusiano baina yetu ukikua zaidi, naihidi kuwa kupitia
Wakurugenzi na Mameneja wetu wa matawi tutaweka utaratibu wa kutembelea
ofisi za Magereza nchi nzima ili kuhakikisha haya tuliyokubaliana hapa
yanatekelezwa”, alisema Dokta Kimei.
BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI
“Nichukue fursa hii kulishukuru Jeshi la Magereza kwa biashara ambayo limekuwa likitupatia, niipongeze SACCOSS ya Magereza kwa uamuzi wa kuwa Wakala wa FahariHuduma, hii si tu itawaongezea kipato kupitia kamisheni za uwakala, pia itasogeza huduma za kibenki karibu na Maaskari Magereza”, alisema Dokta Kimei.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akizungumza katika kikao na uongozi wa Benki ya CRDB, uliomtembelea ofinisi kwake, Makao Makuu ya Magereza jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei.
Akielezea juu ya fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB kwa wafanyakazi Dokta Kimei alisema hivi karibuni Benki imeshusha riba inayo toza katika mikopo binafsi toka 20% mpaka 17%, muda wa marejesho umeongezwa toka miezi 72 hadi miezi 84, wakati kiwango cha kukopa kimeongezwa kutoka shilingi milioni 50 mpaka kufikia Shilingi Milioni 100 hivyo kuwapa wateja wigo mpana zaidi wa kukopa ili kufikia malengo.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (kushoto) akimkabidhi zawadi maalum, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa, wakati alipomtembelea ofisini kwake, Makao Makuu wa Magereza, jijini Dar es salaam, Mei 23, 2018. Mkutano huo ulikuwa na lengo kudumisha uhusiano wa kibiashara baina ya Benki ya CRDB na Jeshi la Magereza nchini.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Dokta Juma Malewa alimshukuru Dokta Kimei kwa kutembelea Jeshi hilo na kuipongeza Benki ya CRDB kwa maboresho hayo katika huduma zake, huku akiisifu zaidi huduma ya Salary Advance ambayo alisema kwa kiasi kikubwa imesaidia kuboresha maisha ya askari. Dokta Malewa alisema katika maboresho hayo yanayoendelea Jeshi la Magereza lingependa kutumia mfumo wa kibenki katika kukusanya mapato yake katika miradi na huduma mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.
“Nikuombe Dokta Kimei na uongozi mzima wa Benki ya CRDB kuona uwezekano wa kuweka huduma za kibenki kama ATM na Matawi kwenye maeneo ya Magereza yenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo”, aliongezea Dokta Malewa. Dokta Malewa pia aliiomba Benki ya CRDB kushiriki katika miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa na Jeshi hilo ikiwamo ujenzi wa hospitali ya Jeshi la Magereza Ukonga, miradi ya Kilimo cha kisasa na chenye tija, mradi wa kokoto Msalato pamoja na uwekezaji katika miradi ya viwanda vidogo vidogo.
Baadhi
ya Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini, wakiongozwa na Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga wa kwanza kulia) wakati
wa kikao maalum na uongozi wa Benki ya CRDB, uliotembelea Makao Makuu ya
Magereza, jijini Dar es salaam leo.
“Ningependa
kuona pia Benki ya CRDB kuwa mteja wa bidhaa na huduma zinazotolewa na
Jeshi la Magereza mfano Benki kutumia samani za ofisi na Magereza kupewa
Kandarasi za ujenzi wa miradi ya Benki inayodhaminiwa au kumilikiwa na
Benki”, aliongezea Dokta Malewa akionyesha fursa ya kibiashara iliyopo
baina ya Benki na Jeshi la Magereza.
Dokta Kimei alimhakikishia Mkuu wa Jeshi la Magereza kuwa Benki ya CRDB ipo tayari kushirikiana na Jeshi hilo katika miradi mbalimbali ambayo wamepanga kuitekeleza, huku akihaahidi kutuma timu ya wataalam kutoka Benki ya CRDB kufanya upembuzi yakinifu juu ya kuweka ATM na kufungua vito vya kutolea huduma katika maeneo ya Jeshi la Magereza ilikufikisha huduma kwa akari kwa urahisi.
Mkurugenzi
wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully
Mwambapa akieleza jambo kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza
nchini, Kamishna Juma Malewa (hayupo pichani) katika kikao
kilichofanyika Makao Makuu ya Magereza, jijini Dar es salaam leo.
BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...