MKUU wa wilaya ya Iringa mkoani Iringa Richard Kasesela ametoa siku saba kujisalimisha kwa wadaiwa sugu vikuwemo vikundi viwili vya vya Mungu ametenda ambavyo kwa pamoja vinadaiwa mkopo wenye thamani ya Zaidi ya million 293,380,925 iliyotolewa na shirika la kuhudumia viwanda vidodo (SIDO) mkoa wa Iringa . 
Akizungumza na wanahabari jana ofisini kwake mkuu huyo wa wilaya ya Iringa ,Kasesela alisema kuwa vikundi namba moja na namba mbili vya Mungu ametenda pekee yake vinadaiwa kiasi cha shilingi milioni 32 wakati wadai sugu wengi wapo katika Manispaa ya Iringa ambao kwa pamoja wanadaiwa kiasi cha shilingi 269,331,225 wakati halmashauri ya Iringa vijijini wanadaiwa 4,858,700 ukiacha wadaiwa wa wengine kutoka wilaya za mkoa wa Iringa . 
 Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa shirika la SIDO ni la umma na lengo lake kuu toka kuanzishwa kwake ni kupanga na kuratibu na kukuza ukuaji ,upanuzi na maendeleo ya viwanda vidogo na vya kati Tanzania bara kwa ajili ya kuwezesha watanzania wengi kupata ajira. Hivyo alisema pamoja na shughuli hizo limekuwa likitoa ushauri wa fedha na mikopo ambayo inalenga kukuza biashara na viwanda vidogo vinavyoanzishwa au vilivyoanzishwa tayari lakini vinahitaji mikopo ili kukua Zaidi. Amesema kutokana na taarifa aliyofikishiwa na meneja wa SIDO mkoa ilionyesha kuna malimbikizo mengi ya mikopo kwa kuwa na wadaiwa sugu wengi Zaidi na pesa nyingi ipo nje . 
 Alisema katika mikopo hiyo ipo mikopo ya mtu moja moja na vikundi na kuwa kwenye taarifa ya SIDO kuna wadaiwa 891 wamelimbikiza jumla ya shilingi 293,380,925 huku wadaiwa binafsi wapo 167 ambao wanadaiwa jumla ya shilingi 181,396,500 na vikundi 15 vyenye wanachama 721 vinavyodaiwa jumla ya shilingi 111,984,425 ndani yake vipo vikundi hivyo viwili vya Mungu ametenda . 
 Hivyo alisema kwa kuanza msako huu utakaosimamiwa na ofisi yake amelazimika kutoa siku 6 hadi jumatatu ijayo mdhamini wa vikundi vya Mungu ametenda awe amejisalimisha pamoja na wanachama wake katika ofisi yake na wadaiwa wengine ndani ya siku saba kuanzia leo Mei 16 wawe wamejisalimisha ofisini kwake na kuanza kurejesha mikopo hiyo . 
 “ Nawaagiza wakopaji wote kupitia vyombo vya habari popote walipo ndani ya wilaya ya Iringa ama mkoa ama wawe nje ya mkoa huu waanze kujisalimisha kwa kulipa madeni kabla ya kutangaza majina yao na picha zao katika vyombo vya habari na wapo wengine ni viongozi wakubwa katika jamii ila katika hili watatusamehe lazima walipe madeni “ 
Meneja wa SIDO mkoa wa Iringa Francisca Simon alisema kuwa wameendelea kuwasaka wakopaji hao kwa kutumia madalali ila baadhi ya madalali wamekuwa si waaminifu badala ya kuwataka wakopaji kulipa mikopo yao kupitia akaunti ya SIDO wamekuwa wakipokea pesa mkononi na kula na kuwa wapo baadhi ya madalali wanawasaka kwa kukiuka taratibu walizokubaliana. 
Pia alisema kukosekana kwa uaminifu kwa baadhi ya madalali kumechangia wakopaji wasumbufu kufanya marejesho kwa wakati na kuwa sasa wameweka dalali mwingine ambaye hatapokea hata senti moja toka kwa wadaiwa hao. 
Ofisa mikopo wa SIDO mkoa wa Iringa Neserian Laizer alisema kuwa mikopo hiyo ya serikali masharti yake huwa nafuu tofauti na mikopo ya taasisi nyingine ila hata hivyo wakopaji huwa wanakuwa na dhamana na kutolea mfano vikundi vya Mungu ametenda ambavyo kiongozi wake aliweka dhamana shamba lake la miti pamoja na nyumba na kuwa mwanzo walifanya vizuri ila mara ya pili wameshindwa kurejesha mikopo hiyo. 
 Alisema kuwa vikundi vya Mungu ametenda ni vikundi ambavyo awali vilikuwa vikifanya vizuri na kukopeshwa zaidi ya mara mbili na kurejesha kwa wakati ila awamu ya mwisho wameshindwa kurejesha kwa madai wanachama wamekimbia
Mkuu wa  wilaya ya Iringa  Richard  Kasesela  akizungumza na wanahabari  leo  ofisini  kwake  kuhusu  wadaiwa  sugu  wa  SIDO  kuanikwa
Mkuu  wa wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  akifafanua  jambo  leo juu ya  wakopaji wa SIDO
Afisa  biashara wa  SIDO  Niko Mahinya  akifafanua  kuhusu  wakopaji  walioshindwa  kurejesha kwa  wakati  mikopo ya  SIDO ,kushoto  ni  meneja  wa  Sido  mkoa  wa Iringa  Francisca Simon
Afisa  mikopo  wa  Sido  mkoa  wa  Iringa Neserian  Laizer  akifafanua  kuhusu  mikopo  ambayo haijarejeshwa  kulia  ni meneja wa  Sido  mkoa  wa Iringa Francisca Simon 
Picha na habari na MatukioDaima TV

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...