Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
NAIBU Waziri wa Afya,Wazee,Jinsia na Watoto na Mbunge wa Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam Dk.Faustine Ndugulile amekabidhi vitanda na magodoro 14 vinavyotarajiwa kuhudumia wagonjwa wa dharula kwenye  Hospitali  ya Vijibweni na kuwataka wataalamu kuvitumia vitanda hivyo kwa lengo lililokusudiwa.

Dk.Ndugulile ameyasema hayo leo wakati akikabidhi vitanda alivyopokea kutoka kwa Jamii ya Australia (Australia Tanzania society) na Kampuni ya JACANA ikiwa ni  matokeo ya mkakati ambayo Serikali inashirikisha sekta binafsi katika hali ya utoaji wa huduma za afya.
Pia amemtaka Mkurugenzi wa Manispa ya Kigamboni na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni  kusimamia mapato na kuhakikisha mifumo ya kudhibiti mapato  inafungwa kwenye vituo vyotevya afya  ili fedha zitakazopatikana zitumike kuboresha huduma nyingine  za afya.
Aidha Dk.Ndugulile amesisitiza ofisi ya Mkurugenzi kuweka mfumo mzuri wa malalamiko ili kuwarahisishia wananchi wanaokuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma kujua waende kwa nani kuweza kuhudumiwa na kusikilizwa malalamiko yao.

"Mkurugenzi Mtendaji,Mganga Mkuu wa Wilaya na Mganga Mfawidhi wekeni tangazo la namba za simu kwenye bango i ili mwananchi akiwa na malalamiko ajue anampigia simu nani, tunataka uwazi na uwajibkaji kwenye serikali ya awamu ya tano,"amesema Dk.Ndugulile.
Pia Naibu Waziri  amesema ni vizuri  Wilaya na  hospitali  kujipanga na kuhakikisha dawa zote za msingi zinakuwepo kwa mujibu wa muongozo na kufafanua Serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka  Sh.Biloni 30 hadi Sh.Bilioni 66.
Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Kigamboni Mh.Faustine Ndugulile akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Vijibweni wakati wa kukabidhi vitanda vya wagonjwa.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh. Hoja Maabad akiwashukuru wafadhili kwa msaada wa vitanda
 Afisa uhusiano  Bw.Ahmed Merere kutoka JACANA akizungumzia lengo la kusaidia Hospitali ya Vijibweni .
 Baadhi ya Vitanda vya kuhudumia wagonjwa wa dharula vilivyokabidhiwa Hospitali ya Vijibweni leo na Naibu Waziri wa Afya.
 kutoka kushoto ni Naibu waziri wa Afya na Mbunge wa Kigamboni Mh.Faustine Ndugulile ,Bw.James Chialo Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society,  Afisa Uhusiano wa JACANA Bw.Ahmed Merere,  Meya wa Manispa

Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Kigamboni Mh.Faustine Ndugulile wa kwanza kushoto akipeana mkono wa shukurani na Afisa Uhusiano wa JACANA wakati wa Makabidhiano ya vitanda.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...