Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas Swami pamoja na viongozi wengine wa jumuia hiyo wa hapa nchini wakati kiongozi huyo alipotembelea Tanzania hivi karibuni. BAPS imetoa kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto 30.

Jumuia ya Kihindu Tanzania (BAPS) imetoa kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo ziatumika kwaajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto wenye matatizo hayo hapa nchini.

Fedha hizo ambazo zitatumika kwaajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 30 wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) zimetolewa hivi karibuni na kaimu kiongozi wa Dunia wa jumuia hiyo.

Akizungumza kuhusu msaada huo Kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu Duniani Mtukutu Bhaktipriyadas Swami alisema wametoa fedha hizo kwa ajili ya kusaidia jamii yenye uhitaji hasa watoto wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi alishukuru kwa msaada huo na kusema kuwa fedha zilizotolewa zitatumika kwa walengwa ambao ni watoto wanaotakiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Prof. Janabi alisema kuwa Taasisi hiyo imekuwa na uhusiano mzuri na Jumuia ya BAPS ambao kila mwaka wamekuwa wakichangia fedha kwaajili ya matibabu ya moyo kwa watoto ambao baada ya matibabu wamepona na wengine wamerudi shuleni kuendelea na masomo yao.

Tangu mwaka 2016 BAPS wamekuwa wakitoa fedha kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto ambapo hadi sasa jumla ya watoto 290 wameshafanyiwa upasuaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisalimiana na kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas Swami alipotembelea Tanzania hivi karibuni. BAPS imetoa kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo zitatumika kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto 30.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Viongozi wa Jumuia ya Kihindu (BAPS) wakijadili jambo wakati Kaimu kiongozi wa Dunia wa Jumuia hiyo Mtukufu Bhaktipriyadas Swami alipotembelea Tanzania hivi karibuni. BAPS imetoa kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo zitatumika kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto 30.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas Swami alipotembelea Tanzania hivi karibuni. Tangu mwaka 2016 BAPS wamekuwa wakitoa fedha kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto ambapo hadi sasa jumla ya watoto 290 wameshafanyiwa upasuaji.
Kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas Swami akimpa zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati kiongozi huyo alipotembelea nchini hivi karibuni. Tangu mwaka 2016 BAPS wamekuwa wakitoa fedha kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto ambapo hadi sasa jumla ya watoto 290 wameshafanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri. Picha na JKCI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...