Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

KAMPUNI za ukandarasi zaidi ya 70 zimeamua kujitolea kujenga mitaro ya barabara mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam bure kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Mkuu wa mkoa huo Paul Makonda.

Hatua hiyo inakuja baada ya Makonda kufanya ziara usiku na mchana kwa lengo la kujionea uharibifu mkubwa wa barabara uliotokana na ukosefu wa mitaro ya maji na kuamua kuwashirikisha wakandarasi hao ambao walipokea kwa mikono miwili ombi hilo. 

Taarifa yake kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam Makonda pia amewaagiza wenyeviti wa mitaa kuratibu idadi ya barabara zisizokuwa na mitaro kwenye mitaa yao kisha kupeleka kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini(TARURA) Wilaya kwa ajili ya kupatiwa kampuni itakayojenga mitaro hiyo. 

Aidha Makonda amezishukuru kampuni zilizojitolea kujenga mitaro hiyo bure jambo litakalosaidia kuokoa mabilion ya fedha za Serikali.

Kwa upande wao wakandarasi wamesema wamejiandaa vizuri kuanzia vifaa na wataalamu kwaajili ya ujenzi huo huku baadhi yao wakiwa tayari wameanza ujenzi kwenye baadhi ya mitaa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakandarasi wa kampuni mbalimbali zilizojitolea kujenga mitaro ya barabara mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam, bure kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Mkuu wa mkoa .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...