Na Sultani Kipingo
Vilabu viwili vya soka vikubwa barani Ulaya leo vinaingia uwanja wa Olimpiysky Stadium jijini Kiev huku Real Madrid wakipania kunyakua kombe la UEFA Champions kwa mara ya 13 - kwa mara ya tatu mfululizo - kwa kuishinda Liverpool FC iiliyoingia fainali kwa mara ya kwanza katika miaka 11 wakiwinda ubingwa huo kwa mara ya sita.
Ushindi huko Kiev utaifanya Real Madrid timu ya nne kushinda mataji matatu ya Ulaya na ya kwanza kufanya hivyo mara mbili, kufuatia ushindi wao wa fainali kati ya miaka 1956 na 1960. Ajax (1971-73) na FC Bayern Munich (1974-76) zikiwa timu pekee zilizoshinda kombe hilo mfululizo.
Zinadine Zidane wa Real Madrid anaweza pia kuwa kocha wa kwanza kushinda makombe ya Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo, akiwa wa kwanza kushinda ligi ya UEFA mfuluizo mwaka 2017.
Mafanikio ya Real Madrid leo yatamaanisha ushindi wa mara tano kwa mara ya kwanza kwa mfungaji bora wa michuano hiyo, Cristian Ronaldo, ambaye pia atakuwa mchezaji wa  tano kushinda  fainali za Ulaya na wa kwanza katika zama za UEFA Champions kama atacheza na timu yake kushinda. Wachezaji wengine ni magwiji watatu wa Real Madrid Paco Gento (mchezaji pekee aliyecheza fainali hizo mara sita), Alfredo Di Stefano na Maria Zarraga pamoja na Paolo Maldini wa AC Milan.
Mchezo huu unakumbushia fainali za kombe la Ulaya mwaka 1981, ambapo Liverpool ilishinda bao 1-0 jijini Paris kuwapa ushindi wa mara ya tatu wa mashindano hayo katika miaka mitano. Hiyo ilikuwa ni mechi ya mwisho kwa Real Madrid kushindwa kwenye michuano hiyo.
Ushindi huo wa Liverpool ni wa pekee kwa timu ya Uingereza dhidi ya timu ya Spain  katika kombe la ubingwa wa Ulaya. Vilabu vya La Liga vimeshinda mara tatu zilizotangulia dhidi ya timu za Uingereza - FC Barcelona ikiifunga Arsenal FC 2-1 mwaka 2006 na Machester United FC mwaka 2009 (2-0) na 2011 (3-1).
Liverpool na Real Madrid wameshakutana mara tano huko nyuma kwenye michuano ya Ulaya, Liverpool wakishinda michezo yao   mitatu na Madrid mara mbili, huku klabu hiyo ya Uingereza ikiwa imefunga magoli sita dhid ya manne ya Madrid.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...