Na Ramadhan Ali - Maelezo
Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imegundua udanganyifu uliokuwa ukifanywa na mfanyabiashara Ujudi Abass wa kubadilisha utambulisho (brand) wa mafuta ya kula ya TURKEY na kuweka utambulisho wa  OKI kinyume na sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ZFDA Dkt. Khamis Ali amesema udanganyifu huo uliokuwa ukifanywa ndani ya Tawi la CCM Makadsara ulibainika baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
Alisema utambulisho wa OKI uliokuwa ukitumiwa  kinyume na sheria na mfanyabiashara huyo ulikuwa wa kughushi na lengo lake kubwa ni kutafuta soka na bei ya juu katika masoko ya Dar e salaam ambako  hivi sasa kunaupungufu wa mafuta hayo.
Dkt. Khamis alisema kuwa mafuta hayo, zaidi ya galoni 747, yanatoka nchini Indonesia na yalizalishwa mwezi Mei mwaka 2017 na muda  wa mwisho wa matimizi ni mwezi Mei mwaka 2019 hivyo yapo salama kwa ajili ya matumizi na kosa la mfanyabiashara huyo ni kubadilisha utambulisho halali wa TURKEY na kuweka utambulisho wa Kampuni nyengine
Alisema mfanyabiashara Ujudi Abss hivi sasa anashikiliwa na vyombo vya ulinzi na  anatarajiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria wakati wowote kujibu tuhuma za udanganyifu.
Mwakilishi wa Kampuni ya Sahara ambao ni wakala wa OKI ameeleza kusikitishwa na kitendo cha  udanganyifu wa  uliofanywa na mfanyabiashara huyo kutumia stika za kampuni hiyo kwa lengo la kutafuta kipato kwa vile mafuta ya OKI ni maarufu na yanasoko.
Alisema kitendo cha kutumia stika ya kampuni kwa biashara nyengine kwa njia  udanganyifu kinaweza kushusha hadhi ya biashara ya halisi na  kupoteza imani kwa watumiaji. 
 KAIMU Mkurugenzi Huduma za  Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Abdulaziz Shaib Moh’d akibandua stika ya kughushi ya OKI iliyowekwa kwenye mageleni ya mafuta ya kula ya kampuni ya TURKEY  katika eneo la Shaurimoyo Mjini Zanzibar.
 BAADHI ya madumu ya  mafuata ya kula kutoka Indonesia yenye stika ya  TURKEY yakiwa  yamepandishiwa  stika ya OKI  kwa njia za udanganyifu bila ya idhini ya wamiliki wa kampuni hiyo.
 VIFAA vilivyotumika kubadilishia Stika za mafuta ya TURKEY kutoka Indonesia na kuwekwa stika ya OKI juu kwa njia za udanganyifu bila ya idhini ya wamiliki wa kampuni hiyo.
 MADUMU ya mafuta ya kula yakiwa  yameshabadiliswa stika ya asili ya TURKEY na kuwekwa ya OKI yakisubiri kuingizwa Sokoni.
  KAIMU Mkurugenzi  Mtendaji Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Khamis Ali Omar akionyesha stika zilizotumika kufanyia udanganyifu  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Mtaa wa Makadara Mjini Zanzibar.
MWAKILISHI wa Kampuni ya Sahara ambao ni Wakala wa Mafuta ya OKI Salum Moh’d akizungumza na Waandishi wa Habari jinsi ya kampuni hiyo ilivyosikitishwa na udanganyifu wa kutumika stika ya kampuni hiyo bila idhini yao.
Na Abdalla Omar / Maelezo Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...