Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kufanya hima maana Serikali iko katika hatua za mwisho za kuanza kufanya mageuzi makubwa katika eneo la mazingira ya biashara kama ilivyobainishwa hivi karibuni na Waziri wa Viwanda na Biashara.


Makamu wa Rais ameyasema hayo  wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) unaotanguliwa na mafunzo endelevu ya Sheria.
“Nawapongeza TAWLA kwa namna ya kipekee sana kwa kutimiza miaka 28 ya uhai wake. Ni miaka 28 ya mafanikio makubwa sana. Nawapongeza kwa sababu, katika miaka 28 ya uhai wenu, hamjawahi kuyumba wala kutoka nje ya lengo la kuanzishwa kwenu, ambalo ni kutumia taaluma ya sheria kuwasaidia wanawake wasio na uwezo kupata msaada wa kisheria na haki zao.” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amesema anatambua na kuguswa na kazi nzuri inayofanywa na Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) hapa nchini ya kupigania haki za wanawake kwa kutumia taaluma ya sheria.Mkutano huo wa mwaka huu ambao umebeba kauli mbiu ya “Uwekezaji Wenye Tija; Kufungua Fursa kwa Mitaji ya Sekta Binafsi na Umma Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi”Makamu wa Rais amewataka Chama Cha Wanasheria Wanawake wawasaidie wanawake wajasiriamali kujua sheria, “Sisi kama wanawake kwanza ni kumnyanyua mwanamke, Ukimnyanyua Mwanamke umeinyanyua Tanzania.”
Makamu wa Rais aliwahakikishia TAWLA kuwa Serikali haina upungufu wa dhamira. “ Serikali yenu inajali na inao utashi wa kumkomboa mwanamke kiuchumi”,Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano maana maslahi ya TAWLA na ya Serikali yanakutana katikati katika suala hili.
Akimkaribisha Makamu wa Rais, Naibu Waziri wa Afya, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile amewataka TAWLA kutumia maendeleo ya kiteknolojia kujitangaza ili wanawake wengi zaidi wapate taarifa zao na kuweza kupata msaada wa kisheria.Nae, Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka amesema TAWLA inapenda kuona mtoto wa kike na mwanamke anaendelea kupewa kipaumbele katika maendeleo ya Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake TANZANIA(TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo Endelevu ya Sheria uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo Endelevu ya Sheria uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa TAWLA Bi. Athanasia Soka wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake TANZANIA(TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo Endelevu ya Sheria uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.




Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile akihutubia kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua mkutano mkuu wa 28 wa TAWLA. 
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...