MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekabidhiwa vifaa vya  ujenzi vyenye thamani ya Sh.milioni 400 kutoka kiwanda cha MMI Steel ltd kwaajili ya kampeni ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam.

Vifaa alivyokabidhiwa ni Mabati 15,000 yenye thamani ya Sh.million 360, nondo tani 22 zenye thamani ya Sh.million 40 ambapo kiwanda hicho kimemuahidi tena kumpatia vifaa vingine ikiwemo rangi, nondo na mabati. 

Akipokea vifaa hivyo leo jijini Dar es Salaam, Makonda ameshukuru kiwanda cha MMI Steel chini ya Mkurugenzi wake Subhash Patel kwa kuwa mdau mkubwa wa kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu na kuwaomba wadau na wananchi kujitokeza kuchangia kampeni hiyo ili kutoa heshima kwa walimu. 

Aidha amesema kampeni ya ujezi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri ambapo hivi karibuni atapokea kontena nyingine 16 za furniture kutoka Marekani, Kontena 10 za Vitabu kwaajili ya Maktaba ya jamii kutoka Marekani, Kontena 10 za vifaa tiba kutoka Uingereza na kontena 10 za Maziwa kutoka China kwaajili ya watoto waliojitokeza wakati wa mchakato wa kutafuta haki ya watoto waliotelekeza kama sehemu ya msaada.

Kwa upande wake Patel amesema wameamua kutoa vifaa hivyo kama sehemu ya kutambua umuhimu wa elimu na kuunga mkono jitiada za RC Makonda katika uboreahaji wa elimu kupitia mazingira bora ya walimu kufanya kazi.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa vifaa mablimbali  kwa ajili  ujenzi wa ofisi za Walimu na kiwanda cha MIN Steel vyenye thamani ya shilingi milioni mia nne.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akiangalia mapati aliyo kabidhiwa na kiwanda cha MMI Siteel kwajili ya kuezekea ofisi za walimu.
 Mkuu wamkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda(katikati) akimshukuru  Mkurugenzi wa Kiwanda cha MMI Steel Ltd,Subhash Patel kwa kuwa mdau mkubwa wa kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu (kulia) Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam,Hamis Lissu.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...