Asema zitasaidia kukomesha utoroshaji wa mifugo nje ya nchi

Na John Mapepele 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ameagiza maeneo yote ya minada ya awali na upili yapimwe na kuwekwa alama za mipaka katika mwaka wa fedha 2018/19 ili kuepuka uvamizi unaofanywa na watumiaji wengine wa ardhi. 

Maelekezo hayo ameyatoa leo kwenye hafla ya iliyofanyika kwenye Ofisi ya Dar es Salaam wakati akikabidhi pikipiki kumi ili zitumike kwenye mipaka na minada ya upili kwa lengo la kudhibiti utoroshaji wa mifugo na mazao yake nje ya nchi. Alisema Serikali inakusudia kuifunga minada yote iliyoanzishwa kiholela kwa nia ovu ambapo amesema kuendelea kubaki kwa minada hiyo kunadhoofisha minada ambayo imeanzishwa kwa kufuata taratibu za Serikali. 

Aidha, Waziri Mpina alisema kuanzia sasa minada yote itaboreshwa na kuwa katika mfumo wa kielektroniki ili kudhibiti mapato ya Serikali kwa njia za kisasa zaidi.“Kuanzia sasa wizara yangu inaingia kwenye mfumo mpya katika kusimamia minada yote ambapo utaiunganisha kwenye mfumo wa kielektroniki” alisisitiza Mpina 

Sambamba na hatua hiyo Mpina amemwagiza Katibu Mkuu anayeshughulikia Sekta ya mifugo Dkt. Mary Mashingo kuhakikisha miundo mbinu ya minada yote inakarabatiwa mara moja na ili kuboresha usimamizi wa sekta ya mifugo nchini.Alisema Wizara inasimamia minada 12 ya upili na 10 ya mipakani ambapo minada ya upili ipo nchi nzima kwa kuzingatia wingi wa mifugo katika eneo husika. 

Mpina alisema hapa nchini kuna minada 465 ya awali ambayo huendeshwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM). Aidha, minada ya mipakani imewekwa kuzingatia njia za kusafirishia mifugo kwenda nje ya nchi. 

Alitaja minada ya upili na Wilaya ilipo kuwa ni Pugu (Ilala), Kizota (Dodoma), Sekenke (Iramba), Igunga (Igunga), Ipuli (Tabora) na Mhunze (Kishapu). Mingine ni Nyamatala (Misungwi), Meserani (Monduli), Themi (Arumeru), Weruweru (Hai), Korogwe (Korogwe) na Lumecha (Songea). Aidha, minada ya mipakani ni pamoja na Buhigwe (Kasulu), Kasesya (Kalambo), Kileo (Mwanga), Kirumi (Butiama), Longido (Longido) na Waso (Ngorongoro). 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina(mwenye miwani) akikagua moja kati ya pikipiki kumi kabla ya kuzikabidhi ili zitumike kwenye minada ya mipakani na upili.Picha na John MapepeleWaziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akikata utepe kwenye moja kati ya pikipiki kumi kabla ya kuzikabidhi ili zitumike kwenye minada ya mipakani na upili.Picha na John MapepeleWaziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akienesha   moja kati ya pikipiki kumi baada ya kuzikabidhi ili zitumike kwenye minada ya mipakani na upili.Picha na John Mapepele.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...