Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii
MSHAMBULIAJI wa Azam Shaaban Idd, amekiri kuwa nje ya dimba kwa takribani
miezi saba akiuguza majeraha ya nyonga kulimwaribia kuendeleza kasi aliyokuwa
nayo msimu uliopita.
Shaaban aliweza kuiongoza Azam FC kuichapa Tanzania Prisons mabao 4-1 kwenye
mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) akifunga hat-trick na jingine
likitupiwa wavuni na kiungo Frank Domayo.
Mara baada ya Shaaban kukosa raundi ya kwanza ya ligi kutokana na majeraha
aliyopata mwishoni mwa msimu uliopita, hivi sasa amerejea vema kabisa baada ya
hat-trick hiyo kumfanya akikishe mabao nane kwenye ligi msimu huu, huku akiandika
rekodi ya kufunga mabao sita ndani ya mechi nne zilizopita.
Mabao hayo nane yamemfanya kuvunja rekodi yake ya msimu uliopita
alipopandishwa timu kubwa akitokea Azam B, na kufunga mabao sita kwenye msimu
wake wa kwanza wa ligi.
Akizungumzia mchezo uliopita, Shaaban alisema ilimlazimu kuvuta subira ili kurejea
kwenye ubora wake na anamshukuru Mwenyezi Mungu hivi sasa ameanza kufanya
vizuri huku akiahidi makubwa zaidi msimu ujao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...