Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw.Antonio Guterres ametangaza uteuzi wa Bi.Joyce Msuya kutoka Tanzania kuwa naibu katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia program ya mazingira yenye makao makuu yake Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa mataifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari leo tarehe 22 Mei, Bi Msuya anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Bw.Ibrahim Thiaw wa Mauritania aliyemaliza muda wake ambaye katibu Mkuu wa umoja wa mataifa amemuelezea kuwa na utumishi uliotukuka katika kipindi chake cha uongozi.

Bi.Joyce Msuya amekua akifanya kazi kama mshauri wa makamu wa rais wa benki ya dunia anayeshughulikia nchi za Asia Mashariki pamoja na ukanda wa Pasifiki tangu mwaka 2017, makao makuu ya benki ya Dunia Washington D.C Marekani.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi.Msuya atatumia muzoefu wake wa miaka 20 katika benki ya Dunia, pamoja na uzoefu wake katika masuala ya maendeleo ya kimataifa katika kazi yake mpya na anaimani kuwa ataleta mabadiliko makubwa katika umoja wa mataifa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Bi.Msuya amewahi kufanya kazi kama mwakilishi maalum wa benki ya Dunia na mkuu wa kundi la benki ya dunia nchini Korea ya kusini,pamoja na mratibu wa taasisi ya benki ya dunia katika Asia Mashariki na ukanda wa Pasifiki ofisi iliyoko China, na ameahi kuwa na nafasi mbalimbali za juu katika benki ya dunia na washirika wake.

Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa Bi.Joyce Msuya ana Shahada ya uzamili ya Maikrobailojia na kinga kutoka Chuo Kikuu cha Ottawa, Canada pamoja na shahada ya Baiokemia kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde,Scotland.

Programu ya umoja wa mataifa ya mazingira ni mpango wa kidunia wa mazingira unaolenga kutoa mwelekeo katika uongozi na usimamizi wa mazingira, na kuwashauri wadau na nchi wanachama kwa ujumla njia sahihi za kutunza na kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Programu ya umoja wa mataifa ya mazingira inafanya kazi na serikali,mashirika na asasi za kimataifa duniani kote. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...