NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mbeya

SERIKALI ilianzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata mafao bora na stahiki ya fidia tofauti na sheria ya zamani iliyotoa viwango vya chini vya fidia, lakini pia kuwawezesha waajiri kupata muda zaidi kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendeshaji.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, jijini Mbeya leo Mei 26, 2018 wakati akifungua mkutano baina ya Serikali na wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.

Mhe. Mvunde alisema viwango vya juu vya malipo ya fidia kwa wafanyakazi walipokuwa wanaumia kazini kabla ya sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ilikuwa ni shilingi 108,000/=kwa mfanyakazi aliyepata ajali au kuumia kazini, lakini pia sheria inasema kulikuwa na malipo mengine ya shilingi 83,000/= kwa mfanyakzi aliyefariki kwa ajali au ugonjwa kutokana na kazi aliyokuwa akifanya na malipo hayo yalitegemea pia mkataba wa ajira yake unasemaje.

“Serikali ilikuja na sheria mpya baada ya kuona viwango hivi kwa ubinadamu na kwa hali halisi, vilikuwa vimepitwa sana na wakati na wafanyakazi walikuwa wanapata fidia hiyo kwa kadhia kubwa sana na viwango hivyo haviendani na ukuaji wa uchumi na kwa wakati tulionao.” Alifafanua Mhe. Naibu Waziri.

Aidha Mhe. Mavunde alisema, Mfuko unafaida kubwa sio tu kwa wafanyakazi bali pia kwa waajiri na taifa kwa ujumla ambapo wafanyakazi sasa wanauhakika wa kupata kinga ya kipato kutoakana na majanga ambayo yatasababishwa na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi wanazofanya, lakini waajiri nao watapata muda zaidi wa kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendelevu wa biashara na shughuli zao kwani Serikali kupitia Mfuko itabeba mzigo wote wa gharama pindi mfanyakazi atakapofikwa na janga lolote awapo kazini.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, akipeana mikono na mama mjane, Atulehemu Kiduko, ambaye analipwa fidia ya kila mwezi kufuatia kifo cha mumewe wakati akiwa kazini kwenye kiwanda cha karatasi Mgololo kilichoko Mufindi mjini Iringa. mama huyo alitoa ushuhuda wa huduma anayopata kutoka WCF wakati wa kutano baina ya Serikali na wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini uliofanyika jijini Mbeya Mei 26, 2018 kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, akifungua mkutano baina ya Serikali na wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini uliofanyika jijinmi Mneya Mei 26, 2018 kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi, akitoa hotuba

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba akizungumza.
Sehemu ya waliohudhuria mkutano huo.
Sehemu ya waliohudhuria mkutano huo.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...