Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa GBRI Co. Ltd Bi Hadija Jabiri kwa mafanikio makubwa aliyopata kupitia kilimo cha mbogamboga.

Aidha amempongeza kwa kuajiri takriban Wafanyakazi 236 sambamba na uanzishwaji wa mpango wa ushikirishwaji wakulima wadogo wadogo(out-growers) ambao wataiuzia Kampuni hiyo mazao mbalimbali ya mboga mboga ili aweze kufikia mahitaji ya soko la nje ambayo ni tani 26 kwa wiki za maharage machanga na njegere changa.

Mavunde ametoa pongezi hizo leo alipofanya ziara fupi kutembelea Mashamba hayo ya Mboga mboga yaliyopo Kijiji cha Kiwele, Halmashauri ya Iringa Vijijini yanayomilikiwa na Bi Hadija Jabiri kijana mdogo mwenye umri wa miaka 27.

Mavunde amesisitiza pia utekelezwaji wa agizo la Waziri Mkuu kwa Tawala za mikoa juu ya utengwaji wa maeneo mahsusi kwa ajili ya shughuli za kiuchumi za Vijana ili Vijana wengi zaidi wapate fursa za maeneo ya kufanyia shughuli mbalimbali na pia kuitaka Mifuko ya Uwezeshwaji Wananchi Kiuchumi kusaidia jitihada hizi za Bi Hadija ili aweze kufikia mahitaji ya soko.

Akitoa taarifa kwa Naibu Waziri Mavunde,Meneja wa PackHouse Bw.Ferdinand Sinkala amesema kwamba Kampuni yao ina soko kubwa la Maharage na Njegere changa katika nchi za Uingereza,Ireland na Sweden lakini changamoto kubwa inayowakabili ni upatikanaji wa ardhi ili kuwa na eneo kubwa zaidi waweze kulima na kukidhi mahitaji ya soko la nje.

Amesema kwa sasa wameamua kuwashirikisha wakulima wadogo wadogo kulima mazao hayo ili waweze kukidhi mahitaji ya soko la tani 26 kwa wiki,lakini pia ameiomba Serikali kuunga mkono jitihada za Vijana walioamua kushiriki katika Kilimo hasa kilimo cha mboga mboga kwa kuwawezesha ili waweze kufikia malengo yao.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akikagua shamba la mboga mboga.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akikabidhiwa mboga mboga.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akiwasikiliza wataalam wa GBRI
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akiwa ameshika maharage machanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa GBRI Co. Ltd Bi Hadija Jabiri 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...