JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Description: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Ndg. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Mei, 2018
amekutana na kufanya mazungumzo na Wenyekiti watatu wa Jumuiya
za CCM, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Wenyeviti hao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Ndg. Edmund
Mndolwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg.
Gaudentia Kabaka na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)
Ndg. Kheri James.
Baada ya mazungumzo hayo viongozi hao wamesema wamekutana na
Ndg. Magufuli na kumueleza kuhusu maendeleo ya Jumuiya zao na kumpa
salamu kutoka kwa Rais wa Afrika Kusini Ndg. Cyril Ramaphosa na Rais wa
Zimbabwe Ndg. Emmerson Mnangagwa pamoja na viongozi wa vyama
tawala vya ANC cha Afrika Kusini na ZANU-PF cha Zimbabwe ambavyo ni
vyama rafiki vya CCM.
“Tumekuja kumueleza ziara yetu ilikuwaje lakini zaidi ya hapo sisi
kama wenyeviti wake wa Jumuiya tumekuja kuzungumza nae ili
tuweze kuendesha jumuiya zetu kwa ufanisi mzuri zaidi” amesema
Ndg. Mndolwa.
“Tumekuja na salamu kutoka kwa Marais wa Afrika Kusini na Zimbabwe,
wanasema wanatuheshimu sana na wanatutegemea sana, pia wametaka
urafiki wa vyama vyetu uendelee” amesema Ndg. Kabaka.
“Tumefikisha salamu za vijana wa CCM kwa vijana wa vyama rafiki
vya ANC na ZANU-PF na kimsingi vijana wa ANC na ZANU-PF wanatambua
mchango mkubwa wa CCM katika kufikisha mataifa yao kwenye mafanikio
makubwa ya uhuru na maendeleo waliyonayo leo” amesema Ndg. Kheri James.
Katika hatua nyingine Ndg. Magufuli amekutana na kufanya
mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu na Mwenyekiti Mstaafu
wa CCM Ndg. Benjamin William Mkapa na Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Bara) Ndg. Philip Mangula, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
25 Mei, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa (kushoto) pamoja na Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara Philip Mangula Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa (kulia) pamoja na Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara Phillip Mangula (kushoto) mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Dkt. Edmund Mndolwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Dkt. Edmund Mndolwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa   Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Dkt. Edmund Mndolwa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...