THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

RC KIGOMA AWAPONGEZA VIJANA WALIOHITIMU MAFUNZO YA JKT KATIKA KIKOSI CHA KJ 824 KWA AANDIKO LAO LA KUTENGENEZA SABUNI

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Kikosi cha KJ 824 Kanembwa wilayani Kakonko Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Amosi Mollo amewapongeza vijana wa oparesheni Melelani walio hitimu mafunzo ya awali ya Jeshi la Kujenga Taifa( Jkt ) kwa andiko walilolifanyia kazi la utengenezaji wa sabuni ambalo litapelekea kuanzishwa kiwanda cha utengenezaji wa sabuni kikosini hapo.

Akizungumza jana wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi kwa vijana 732 wanaojitolea yaliyofanyika kwa miezi mitano, Mollo amesema katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Awamu ya tano wameandaa mpango wa kuanzisha kiwanda cha sabuni za kufulia.

Pia sabuni za kuogea na kunawia mikono ilikuhakikisha falsafa waliyowafundisha vijana hao ya kujitegemea katika ujasiriamali kwa kuwa vijana hao wamemaliza mafunzo ya awali wataendelea kujifunza stadi za maisha wakiwa kambini hapo.

Amesema anawapongeza vijana hao kwa kujitolea kuandaa andiko la utengenezaji wa sabuni ambalo wameanza kulifanyia kazi na sasa linaingiza pato kwa Jeshi la Kujenga Taifa ambapo ni matokeo mazuri ya kujifunza na kutumia elimu walioipata ya ujasiriamali, uzalendo, kujituma na kujitegemea inayotolewa kambini hapo kuhakikisha wanaondokana na falsafa ya kwamba hakuna ajira jambo ambalo limekuwa wimbo kwa vijana wengi mitaani.

Amesema nje na utengenezaji wa sabuni kikosi hicho kinajihusisha na ukulima wa alizeti, mahindi, kahawa na ufugaji wa nyuki na uchakataji wa asali, ufugaji wa mifugo mbalimbali na utengenezaji wa mafuta ya kupikia ya Alizeti.Amesema lengo ikiwa ni kuwajenga vijana wanaoingia kambini hapo kwa ajili ya mafunzo kuanza kujifunza namna ya ujasiliamali na kujitegemea hata watakapo rudi uraiani wakawe mfano na fundisho kwa vijana wenzao .

Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuja kujifunza namna ya ujasiliamali kikosini hapo, na kuwataka vijana walio hitimu mafunzo hayo kutumia mafunzo hayo kulinda amani ya Nchi na kujishughulisha katika shughuli za maendeleo ili kuondokana na umasikini uliopo katika familia zao.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika sherehe hiyo Mkuu wa wilaya ya Kibondo Louis Bura aliwapongeza wakufunzi wa kikosi hicho kwa kazi kubwa walioifanya ya kuwanoa wahitimu hayo na kuwataka vijana kuyaishi yale mema yote waliojifunza pamoja na mafunzo waliyo yapata waendelee kuonesha nidhamu na utii watakapo endelea kuwepo kambini hapo.

Aidha alimuomba mkuu wa kikosi kuhakikisha anatafuta soko la kuuza bidhaa hizo ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wakurugenzi wa halmashauri kununua sabuni za kusafishia vyoo na kunawia mikono katika kambi hiyo ili kuuunga Mkono jitihada za vijana na jeshi la kujenga taifa.

"Ntoe pongezi zangu za dhati kwa wakufunzi wote najua mnafanya kazi katika mazingira magumu lakini kwa uzalendo mlionao mmehakikisha vijana wetu wAnajifunza namna bora ya maisha ikiwa ni pamoja na ujasili, uzalendo wa kujitoa kwa ajili ya Nchi yetu pamoja na ujasiliamali hii ndiyo falsafa tuliyo achiwa na waasisi wetu", alisema Bura.

Akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi mmoja wa Wahitimu hao Deogratiusi Mgaya amesema mafunzo hayo yamewajenga kuwa wazalendo na walipoanza mafunzo hayo walianza vijana 739 baadhi ya hao walishindwa kumaliza mafunzo yao kwa sababu ya Kifo cha mwenzao mmoja na utoro wa baadhi na kupelekea idadi ya walio hitimu kuwa 732 ambao wamepata mafunzo hayo ya awali.

Hata hivyo amewaomba wazazi kuwahimiza watoto wao kuingia jeshi la kujenga taifa ili kuwafanya vijana kuwa wazalendo na kuepukana na vitendo viovu pamoja na kujijenga katika kutegemea kujiajiri wenyewe na bila kusubili mpaka Serikali itoe ajira kwao.