Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Zogowale ,mjini Kibaha Mkoani Pwani ,wakishangilia kupata huduma ya maji shuleni hapo ,baada ya kujengewa kisima cha kupampu kilichogharimu zaidi ya sh.mil.11 ,(wa katikati)Mkurugenzi wa Rehema Foundation ,Mohammed Cesur.

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

CHANGAMOTO ya maji safi iliyokuwa ikiwakabili wanafunzi wa shule ya sekondari Zogowale, Mjini Kibaha mkoani Pwani, inabaki historia baada ya kujengewa kisima kirefu cha kupampu, kilichogharimu zaidi ya sh. mil 11, kwa msaada kutoka taasisi ya Rehema.

Licha ya hilo, shule hiyo bado inakabiliwa na kero kubwa ya ukosefu wa uzio hali inayotishia usalama kwa wanafunzi na walimu. Akizungumza wakati wa makabidhiano ya kisima hicho ,kaimu mkurugenzi wa Rehema Foundation ,Rafii Jongo ,alisema ujenzi wa kisima hicho umekamika kwa wiki mbili .

Alielezea ,taasisi hiyo inajihusisha na masuala ya kijamii na hadi sasa imeshasaidia kuchimba visima ndani ya jamii 185 Tanzania Bara na Visiwani ambapo kwa mkoa wa Pwani imechimba visima 50.# "Tunatoa pia misaada ya chakula na kugawa nyama ya ng'ombe kwa watu wasiojiweza nyakati za mfungo tatu ,Na kila mwaka tunachinja ng'ombe 1,000, tunapeleka watanzania kusoma masomo mbalimbali nchini Uturuki" alisema Jongo .

Nae Mkurugenzi wa taasisi hiyo ,Mohammed Cesur aliwataka wanafunzi watunze kisima hicho kwa ajili ya manufaa ya shule na jamii inayowazunguka. Aliwaasa wanafunzi wajitahidi kusoma ili kuinua taaluma zao . Cesur alisema, changamoto ya maji itakuwa imekwisha hivyo anaamini wanafunzi hao wataelekeza juhudi zao katika masomo .

Kwa upande wake ,mkuu wa shule ya sekondari ya Zogowale ,Tatu Mwambala alisema awali walikuwa wakitumia visima vilivyopo nje ya shule na katika mradi wa kijiji . Alisema maji yalikuwa si ya uhakika na sio salama ambako walipoteza muda kutafuta maji . Tatu alielezea ,ipo changamoto nyingine kubwa ya ukosefu wa uzio hali inayosababisha kushindwa kuwa na usalama wa kutosha.

"Tumeanza kujenga uzio kwa jitihada za wazazi na jamii ,tumekwama kifedha ,tunaomba wadau watusaidie kwa ari na mali kumalizia ujenzi huo " "Shule hii ina wanafunzi wa kike ambapo inatakiwa wawe kwenye usalama zaidi kuliko shule kuwa haina uzio"alisisitiza Tatu .

Mwanafunzi wa kidato cha tano shuleni hapo ,Shamim Shomvi alisema, walikuwa wakipata shida ya maji na kusababisha kutumia muda mwingi kwenda kutafuta huduma hiyo badala ya kujisomea. Alisema, walitumia maji ya visima vya chini ambayo hayakuwa salama, " wanafunzi wengine waliugua magonjwa ya matumbo kama typhoid". Shamim aliwashukuru Rehema Foundation, na kuwaomba wasisite kuwasaidia kutatua matatizo mengine yanayowakabili . Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Jennifer Omolo aliwasihi kuutunza mradi huo ili udumu katika kipindi kirefu.
Baadhi ya viongozi wa shule ya sekondari Zogowale ,serikali ya mtaa wa Zogowale na halmashauri ya Mji wa Kibaha wakiwa pamoja na mkurugenzi wa taasisi ya Rehema Foundation ,Mohammed Cesur ,wakifurahia uzinduzi wa mradi wa maji shuleni hapo ,baada ya kujengewa kisima cha kupampu kilichogharimu zaidi ya sh.mil.11.
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Zogowale Tatu Mwambala, akishukuru baada ya kupokea mradi wa maji shuleni hapo uliojengwa kwa msaada wa taasisi ya Rehema Foundation. (Picha na Mwamvua Mwinyi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...