JOSEPH MPANGALA,MTWARA
Serikali
imesema imekamilisha ujenzi wa Bomba la gas utakoyoiwezesha kampuni ya
kuzalisha saruji ya Dangote iliyopo mkoani Mtwara ambayo inataraji
kuzalisha umeme wa megawatts 35 ambazo zitatumika kwa ajili ya matumizi
ya Kiwanda Hicho.
Akiongea
mara baada ya kutembelea plants ya Kuzalisha umeme ambayo inatarajia
kukamilika mwishoni mwa mwezi huu waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani
amesema kuwa tayari serikali ipo tayari kwa ajili ya kutoa nishati ya
Gas ili kampuni ya Dangote kuweza kuzalisha umeme.
“Na
mm nawaambia tena TPDC wakichelewa baada ya mezi kuisha wakumbushe kwa
barua ili lieleweke kama nani anayechelewa lakini sio wanachelewa kwa
makusudi bali wanamaandalizi yao wenyewe lakini sisi kwa upande wetu
kama serikali tupo tayari hata kama wangetaka leo jioni watachukua gas
ili waendelee kwa hiyo nilitaka kuliweka hili Vizuri kwamba tumeendelea
vizuri kati ya TPDC na Dangote”
Lakini
naye Mhandisi wa kampuni ya BQ Cntractors Limited John Bura anasema
Dangote ataendelea kununua nishati ya Gas zaidi ambapo kufikia mwisho wa
mwezi June Mtambo itakuwa umekamilika tayari kwa kuanza kwa uzalishaji
wa Saruji ambapo ni umbali wa kilomita 2.7 kufikia kiwandani
Aidha
ameongeza kuwa kwa sasa uzalishaji wa saruji ni asilimia 50 lakini
kukamika kwa ujenzi huo kutawezesha kampuni ya dangote kuzalisha saruji
mifuko lakimoja na Nusu kwa siku.
Meneja Mkuu wa GASCO Mhandisi Baltazari T.Mrosso akimuonesha waziri wa Nishati Dk.Medard Kelamani Bomba la Gas linalopeleka Nishati hiyo katika Kiwanda cha Umeme cha Dangote.
Waziri wa Nishati Dr.Medard Kelamani akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kiwanda cha kuchakata Gas na Bomba la Gas Linaloelekea Kiwanda cha saruji Cha dangote.
Waziri wa Nishati na madini Dr Medard Kelamani akiongea na Mkurugenzi wa kiwanda cha Dangote Alhaji Sada ladeubaki mara baada ya kutembelea ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha umeme utakaopelekwa katika kiwanda cha Dangote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...