SERIKALI imewaasa viongozi wa dini waeuepuke migogoro ya mara kwa mara katika Makanisa yao na badala yake waendelee kuwajenga waumini wao wakue kiroho na kujenga dhana ya umoja na upendo katika Taifa.

Pia imesema inawashukuru viongozi wa dini na madhehebu yote ya dini kwa kuendelea kuiombea nchi amani, mshikamano na utulivu, jambo ambalo linaongeza chachu kubwa kufikia mafanikio ya maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Hayo yamesemwa leo (Jumapili, Mei 20, 2018) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika ibada ya kutawazwa Askofu Dkt. Maimbo Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga kuwa Askofu Mkuu wa saba wa Kanisa la Anglikana Tanzania. Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Dayosisi ya Central Tanganyika Jijini Dodoma.

“Nawaombeni wote kwa ujumla wetu, tuendelee kutumia Makanisa yetu kuombea Taifa hili ili tuendelee kuishi kwa amani, upendo na mshikamano”. Watu wa Mungu ni watu wa Upendo, watu wa Mungu ni watu wa amani, watu wa Mungu ni watu wa kiroho”.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa “haitarajiwi kuona watu wa Mungu wakiwa katika mstari wa mbele kuchochea migogoro, kuvunja amani ya Kanisa na kuongoza makundi yanayopingana katika kazi ya Bwana”.Amesema jukumu la makanisa ni kuwajenga waumini kukua kiroho, na kazi ya kuwaongoza watu wamjue Mwenyezi Mungu, ambapo amewaomba imani yao iwe moja na matendo yao yafanane na yale ya Kristo Yesu wanayemuamini.

Waziri Mkuu amesema kuwa nchi haiwezi kupata mafanikio ya kiuchumi na kijamii bila kuilinda amani iliyopo, hivyo amewaomba warejee kumbusho la maandiko Matakatifu katika Waebrania 12:14 “Tatufeni kwa bidii kuwa na Amani na watu wote”.

Pia Waziri Mkuu ametoa wito kwa viongozi hao na wananchi kwa ujumla waendelee kuwaombea viongozi wa Tanzania hususani Rais Dkt. John Magufuli, kuendelea kuwa na afya njema, busara, upendo, hekima katika kuiongoza nchi yetu.

Waziri Mkuu ambaye amemuwakilisha Rais Dkt. Magufuli katika ibada hiyo amesema Serikali inatambua ushirikiano uliopo kati ya madhehebu mbalimbali ya dini nchini kwa ujumla wake na kwamba ushirikiano huo ni wa kihistoria.
 Askofu Mkuu wa saba wa Kanisa la Anglikana Tanzania,  Maimbo Fabian Mndolwa  akila kiapo wakati alipotawazwa  kuw Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, jijini Dodoma, Mei 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikan Tanzania, Jaco Chimeldya katika  sherehe ya kumtawaza Askofu Mkuu wa Saba wa kanisa hilo, Maimbo Fabian Mdolwa  jijini Dodoma, Mei 20,2018. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika sherehe hiyo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza katika  Rais John Pombe Magufuli kwenye sherehe ya kumtawaza Askofu Mkuu wa saba, Maimbo Fabian Mndolwa, jijini Dodoma, Mei 20, 2018.2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa saba wa Kanisa la Anglikana Tanzania,  Maimbo Fabian Mndolwa  baada ya Askofu huyo kutawazwa kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, jijini Dodoma, Mei 20, 2018, kulia ni mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa. Waziri Mkuu alimwakilisha  Rais John Pombe Magufuli.
 Spika wa Bunge Job Ndugai akisalimiana na Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania , Oscar Mnunga katika sherehe ya kumtawaza Askofu  Mkuu wa Saba wa kanisa hilo, Maimbo Fabian Mndolwa  jijini Dodoma, Mei 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...