Na Mwandishi wetu Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeawataka wadau wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kuendelea kutekeleza Sera mbalimbali zilizo chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii katika utekelezaji wa majukumu yao.
Hayo yamesemwa Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye pia ni Mkurugenzi na Msajili wa NGOs Bw. Marcel Katemba Jijini Dodoma wakati wa Kikao kati ya Serikali na Wadau hao kinachokaa kwa siku moja kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi zao na kutekeleza Sera zilizo chini Idara kuu Maendeleo Jamii.
Ameongeza kuwa katika kutekeleza Sera mbalimbali Serikali inashirikiana na Wadau mbalimbali wa maendeleo nchini ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Amesema kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanafanya kazi kubwa nchini katika kuleta maendelo ya jamii na Taifa katika sekta mbalimbali nchini.
“Wadau wa NGOs mnafanya kazi nzuri na kubwa katika kuleta matokeo chanya kwa jamii na taifa letu” alisisitiza Bw.Katemba.
Kwa upande wake Mwakilishi Kutoka Shirika la World Vision Tanzania Bi. Janeth Edson akitoa mrejesho wa makubaliano kati ya Serikali na NGOs kwa upande wa NGOs amesema kuwa wao kama wadau wataendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza Sera mbalimbali na kuwaasa wadau kuendelea kuunganisha nguvu na Serikali katika kusogeza mbele gurudumu la maendeleo.
Mkurugenzi na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel
Katemba akizungumza na wadau Mashirika yasiyo ya Kiserikali
yanayotekeleza Sera zilizo chini ya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii
Jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Msaidizi Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi Tausi Mwilima
(kulia) akieleza yatokanayo na kikao kilichopita kati ya Serikali na
wadau wa NGOs wanaotekeleza Sera mbalimbali zilizo chini ya Idara Kuu
Maendeleo ya Jamii Jijini Dodoma.
Mwakilishi
kutoka Shirika la World Vision Tanzania Bi Janeth Edson akitoa taarifa
kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa hati ya makubaliano ya utekelezaji wa
Sera mbalimbali baina ya Serikali na NGOs kwa upande wa NGOs katika
kikao kati ya Serikali na wadau hao Jijini Dodoma.
Baadhi
ya wajumbe wa Menejimenti ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii na wadau wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa
zikitolewa katika kikao kati ya Serikali na wadau wa NGOs Jijini Dodoma.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...