*Waziri Mwijage asema Taifa limepata pigo kubwa kwa kupoteza watumishi waadilifu.
*Mkurugenzi Mtendaji TIC aelezea utendaji wao, azungumzia namna alivyowaamini.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
Ni vilio na simanzi ndivyo vilivyokuwa vimetawala katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga miili ya watumishi wa tatu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) waliofariki dunia kwa ajali ya gari wakitokea Dar es Salaam kwenda Dodoma kikazi.

Miili hiyo ilifikishwa kwenye viwanja hivyo saa nne asubuhi leo ambapo mamia ya waombolezaji walioongozwa na Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwigaje.Wengine ni  Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali Serikali.

Watumishi hao wa TIC ambao miili yao imeagwa leo viwanjani hapo ni aliyekuwa Mkurugenzi Idara ya Utafiti,Mipango na Mifumo ya Mawasiliano Said Amiri Moshi, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za kitaasisi Zacharia Kingu Meneja Utafiti Martin Masalu

Akizungumza mbele ya mamia ya waombolezaji,Waziri Mwijage amesema vifo vya watumishi hao ni pigo kubwa kwa TIC, Taifa na familia kwa ujumla na enzi za uhai wao walikuwa vijana walioonesha umahiri mkubwa wa kiutumishi.

Amesema kwake yeye watumishi hao walikuwa ni marafiki zake na anachoweza kukilezea  anatambua mchango wa kila mmoja wao kutokana na utendaji kazi wa kizalendo  waliouonesha kwenye kituo hicho.

Amesema waliaminiwa na kupewa majukumu makubwa hasa kwa kuzingatia walikuwa na uelewa mkubwa kuhusu masuala ya uwekezaji.

"Nikiri vijana hao wameacha pigo kubwa kwetu hasa kipindi hiki ambacho tupo kwenye mchakato wa ujenzi wa viwanda nchini.Hata hivyo vijana wengine waliobakia TIC waendelea kutekeleza majukumu yao kwa maslahi ya nchi yetu.

 "Watumishi hawa ambao leo tunawaaga walifariki wakiwa njiani kelekea Dodoma kwa ajili ya kutekeleza majukumu muhimu.Tunafahamu kuna baadhi ya changamoto  ambazo zipo kwenye uwekezaji hivyo walikuwa wanakwenda kwenye kikao kuwaambia watendaji wa Serikali mambo muhimu ya kuvutia uwekezaji nchini,"amesema.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza jambo kwa ndugu na jamaa wa marehemu wakati kuagwa kwa miili ya watumishi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kwenye ukumbi wa Kareemjee jijini  Dar es Salaam.
MkurugenziMtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Geoffrey Mwambe akizungumza na mbele ya waombolezaji walioshiriki kuaga miili ya watumishi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kwenye ukumbi wa Kareemjee jijini  Dar es Salaam.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Hamphrey Polepole akitoa neo la pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu wakati wa kuagwa kwa miili ya wafanyakazi wa TIC.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akitoa heshima ya mwisho kwenye miili ya watumishi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC).
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola akiaga  miili ya watumishi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC)
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Hamphrey Polepole akitoa heshima za mwisho kwenye miili ya watumishi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC)
Mkurugenzi Mtendaji wa Zamani  wa TIC na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari(katikati) akiaga miili ya wafanyakazi wa TIC.
 Wafanyakazi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) wakitoa salamu za pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu waliofariki dunia kwa ajali ya gari wakitokea Dar es Salaam kwenda Dodoma kikazi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...