Na Mwandishi wetu
Benki ya Standard Chartered jana ilizindua awamu ya tatu  ya michuano ya soka ya kuwania kombe lake. Michuano hiyo ya kuwania kombe la Standard Chartered 2018 huchezwa kwa dakika 10 kila upande ukicheza kwa dakika 5. Michunao hiyo inasaka timu itakayoenda kushuhudia kipute kinachopigwa na timu ya Liverpoool. Hii ni mara ya tatu kwa michuano hiyo ya kusisimua kufanyika katika ardhi ya Tanzania kuanzia mwaka 2010.

The Standard Chartered Group ndio wadhamini wakubwa wa Liverpool Football Club kuanzia mwaka 2010 hadi  2018/2019. Kwa kushirikiana na klabu hiyo benki ya Standard huendesha mashindano ya soka ya dakika 10 katika masoko yake makubwa ya Bara la Asia, Afrika na Mashariki ya kati. 

Pia michuano hiyo inawezesha kuchangia katika kuendeleza soka. Ikiwa katika mwaka wake wa saba tangu kuanzishwa kwake katika masoko hayo, mashindano hayo yameendelea kuwa na nguvu zaidi kukiwa na washindi kutoka maeneo mbalimbali ya dunia.

Kenya ilitwaa ushindi mwaka 2016, Korea kusini (2015), Vietnam (2014), Thailand (2013) na Singapore (2012). Michuano hiyo kwa kaiwada ina sehemu tatu kuanzia nchi wenyeji, kikanda na fainali zake hufanyika viwanda vya Anfield – Uingereza. Mwaka huu benki hiyo imebadili mfumo wa michuano na kwamba mshindi atapata tuzo na kwenda Anfield.

Akizungumza wakati wa uzinduzi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Bank nchini Tanzania, Bw. Sanjay Rughani, alisema kwamba mwaka huu kutakuwa tofauti na kwamba mshindi wa mashindano ya ndani yenye timu 32 atatwaa kombe na  kwenda kuangalia mtanange wa ligi kuu ya England.

Timu zitakazoshiriki ni pamoja na wateja wa benki hiyo na michuano hiyo itaanza Juni 23 mwaka huu. Mwaka jana mashindano hayo yalikuwa ya kikanda ambapo timu kutoka Tanzania, Kenya na Uganda zilichuana vikali na timu ya Tanzania ya Azania – Mikoani Traders  walishinda na kwenda kwenye fainali Anfield.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba akitoa utambulisho kwa meza kuu wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia kwenda kushoto ni Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa Kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu, Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo, Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani ( wa pili kushoto) akizungumzia ziara ya nyota na nahodha wa zamani wa Liverpool, Sami Hyypia anayetarajiwa kutua nchini Juni 20 wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu akielezea kuhusu safari yao ya Anfield ambapo aliongeza na kusema amefurahishwa na msimu huu ambapo mashindano hayo hayashirikisha timu za nchi jirani wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo akizungumzia  ujio wa Hyypia ambapo alisema ni nafasi adhimu kwa timu yake kunolewa na nahodha huyo wakati wakijiandaa na mashindano ya mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana, katika mkutano na waandishi wa habari kwenye hafla fupi iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) ya uzinduzi wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (kulia) akitoa salamu za TFF ambapo aliipongeza benki ya Standard Chartered nchini kwa kuinua soka la Tanzania kimataifa kupitia mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 wakati wa sherehe za uzinduzi wa mashinano hayo zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani na kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba.
Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (wa kwanza kushoto) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani ( kushoto) wakizundua sanamu ya nyota na nahodha wa Liverpool, Sami Hyypia anayetarajiwa kutua nchini Juni 20 wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba ( wa kwanza kulia), Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu (wa pili kushoto) pamoja na Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo (wa tatu kulia).
Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (wa kwanza kushoto), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani ( kushoto), Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba (wa kwanza kulia), Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu (wa pili kushoto) pamoja na Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo (wa tatu kulia) wakipata picha ya ukumbusho baada ya kuzindua sanamu ya nyota na nahodha wa Liverpool, Sami Hyypia anayetarajiwa kutua nchini Juni 20 wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya waandishi wa habari na wadau wa michezo waliohudhuria wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...