Taasisi ya Uhusiano wa Umma Tanzania, (PRST) inatarajia kufanya maadhimisho ya wiki ya Mawasiliano Afrika, iliyoanza tokea Mei 21 na kilele chake kinatarajiwa kuwa Mei 25, 2018 na Tanzania watafanyia kwenye Ofisi ndogo ya Bunge iliyopo Posta Jijini Dar es Salaam. 

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa Chama hicho hapa Tanzania, Ndege Makura, amesema ili kufanikisha siku hiyo wameamua kuweka mezani maada inayoendana na agenda kuu ya siku hiyo Kitataifa ya Uchumi wa pamoja barani Afrika, wao wamekuja na Tanzania ya Viwanda. 

 Amesema takribani ya Mataifa yote yamekua katika kusherekea siku hiyo ya mawasiliano ambapo jumla ya miji 60 Barani Afrika wanasherekea ikiwemo na Tanzania. Aidha amesema kuwa katika kongamano hilo, yapo malengo bainishwa Kimataifa huku Bara la Afrika wakijadili uchumi wa pamoja lakini kwa Tanzania watajadili suala la mchango wa Maafisa Uhusiano wa Umma ni kwa jinsi gani wanaweza kuchangia kuleta maendeleo ya uchumi hususani katika suala zima la kutangaza sera ya Tanzania ya Viwanda. 

 "Hii ni siku muhimu kwetu watu wa Uhusiano wa Umma , kwani tutajadili vitu vingi vinavyotokana na Sera za maendeleo ya Taifa, wapo watu wengi hawaelewi nini maana ya Viwanda, dhumuni lake na njia za kufikia ndoto hiyo ya Rais wetu, hata Bungeni tumeona Wabunge wakikinzana kuhusu viwanda, tunaleta mjadala huu ili kujadili kwa kina na wataalamu wetu , Wizara ya Viwanda, Afisa uhusiano wa umma kutoka Serikalini na Taasisi binafsi, waandishi wa habari, ili kusaidia ndoto ya Taifa letu kufikia malengo ya Tanzania ya viwanda ifikapo 2025" amesema Makura. 
Katibu wa Taasisi ya Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) Ndege Makura, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Mei 22, 2018 jijini Dar es Salaam wakati akielezea maadhimisho ya wiki ya Mawasiliano Afrika inayotarajiwa kufanyika katika Ofisi ndogo ya Bunge iliyopo Posta. Pembeni yake ni Rais wa PRST, Loth Makuza.
Rais wa Taasisi ya Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST), Loth Makuza akitoa msisitizo kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono katika maadhimisho ya wiki ya Mawasiliano Afrika inayotarajiwa kufanyika katika Ofisi ndogo ya Bunge iliyopo Posta. Kushoto ni Katibu wa PRST, Ndege Makura. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...