Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) limemuomba Rais Dk.John Magufuli  kuwakabidhiwa Kombe la CECAFA vijana wa chini wa miaka 17 kwa lengo la kuwapa hamasa vijana hao.

Ombi hilo limesemwa leo jijini Dar es Salaam na Rais wa TFF Walaace Karia wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Makao makuu ya Shirikisho hilo. Karia amesema kuwa,wamezunguza na Waziri wa Habari,Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe na tayari ameshaandika barua kwenda kwa Rais Magufuli ili kumpa taarifa ya hafla hiyo itakayofanyika Jumamosi Uwanja wa Taifa.

Mbali na hilo TFF wamemuomba Dk. Magufuli kuwa mgeni rasmi katika mchezo Simba SC dhidi ya Kagera Sugar FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mei 19 mwaka 2018.

Kwa mujibu wa Rais (TFF),Karia, amesema wamemwandikia barua Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk.Harrison Mwakyembe yenye ombi la kumuhitaji Magufuli juu ya ugeni huo. Karia ameeleza kuwa Rais Magufuli atapata wasaa wa kukabidhi kombe la 19 mabingwa wapya wa Ligi Kuu msimu huu wa 2017/18 ambalo wamelipata wakiwa hawajapoteza mchezo wowote msimu huu.

Mbali na Simba kukabidhiwa taji hilo katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Magufuli atawakabidhi pia vijana wa Serengeti Boys Kombe la CEFACA chini ya miaka 17 walilolitwaa nchini Burundi baada ya kuifunga Somalia kwa mabao 2-0 kwenye mechi ya fainali iliyopigwa Uwanja wa Ngozi, jijini Bujumbura.

Sherehe za Simba na Serengeti Boys zitaanza saa 8 mchana huku viiingilio vya mchezo huo (Simba SC vs Kagera Sugar) vikiwa ni 15,000 kwa VIP A, 7000 kwa VIP B na C pia 3000 kwa sehemu ya mzunguko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...