Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepata tuzo ya mshindi wa tatu wa masuala ya usalama na afya sehemu ya kazi (OSHA) kwenye maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahali pa kazi yanayofanyika Mkoani Iringa.

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa TPA wakati wa maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi duniani yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya kichangani mjini Iringa. 
 Waziri wa Kazi, Vijana,  Ajira, Jinsia, Wazee, Watoto na Walemavu, Mhe Jenista Mhagama  akitoa tuzo ya mshindi wa tatu wa tuzo za OSHA za masuala ya usalama na afya sehemu ya kazi kwa Mwakilishi wa TPA, Abiduna Athumani katika maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi duniani yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya kichangani mjini  Iringa.

Mwakilishi wa TPA, Abiduna Athumani akionesha cheti walichotunukiwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi duniani yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya kichangani mjini  Iringa.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akizungumza na Mkaguzi wa Zimamoto, Usalama, Afya  na Mazingira wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Bw.  Dunstan Biyengo mara baada ya kutembelea banda la TPA kwenye maonyesho  OSHA wakati wa maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi duniani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...