Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa wameshiriki katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Ubalozi wa Kuwait kwa ajili ya wananchi wa wilaya hiyo. 

Futari hiyo ilifanyika katika msikiti wa Daaru Salaam Kigamboni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini na wananchi, na kuwajumuisha wanafunzi na mayatima wanaofadhiliwa na jumuiya za misaada za Kuwait zilizopo nchini.
Pembezoni mwa futari hiyo iliyotumbuizwa na kasida kutoka kwa watoto, Al-Najem alimkabidhi Mkuu wa Wilaya wa Kigamboni Hashim Mgandilwa zawadi.
Yafaa kueleza kuwa Ubalozi  wa Kuwait nchini utaendelea na program yake ya kufuturisha katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa  Ramadhan katika maeneo mbalimbali nchini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...