WABUNGE wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara, wameimwagia sifa Serikali hususan Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme TANESCO kufuatia kumaliza adha ya umeme iliyodumu kwa takriban miaka 10 kwenye mikoa hiyo.

Pongezi hizo wamezitoa mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, baada ya kuzindua Kituo cha Kuzalisha umeme wa gesi asilia (Mtwara Gas Plant), mkoani Mtwara Alasiri ya Mei 21, 2018.

Wa kwanza kutoa pongezi hizo alikuwa Mbunge wa Mtwara Mjini kupitia chama cha Wananchi CUF, Mhe Maftah Nachuma ambaye yeye alienda mbali zaidi na kufikia kusema atamuandalia Mhe. Waziri Mkuu mkutano mkubwa wa hadhara ili kuwaeleza wananchi wa jimbo lake, mafanikio yaliyoletwa na serikali.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, leo ninayofuraha kubwa sana, kwani kilio cha muda mrefu cha wana Mtwara, cha kukosa umeme wa uhakika, hatimaye kimepatiwa ufumbuzi na kwetu sisi hii ni sherehe kubwa, ningetamani mkutano huu ungewaalika na viongozi wengine wa vyama vya siasa, na mimi binafsi nitakuandalia mkutano mkubwa wa hadhara ili uje uwaeleze wananchi maendeleo haya yaliyoletwa na serikali.” Alisema Mhe. Nachuma.

Naye Mwenyekiti wa wabunge kutoka Mkoa wa Lindi, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini, Mhe. Selemani Bungara, alisema maendeleo haya ambayo serikali inawafikishia wananchi ni kwa sababu bunge linaisimamia vema serikali.“Siku zote tunasema Kusini kwanza mambo mengine baadaye, na mimi niwaambie, tutaendelea kupiga kelele hadi kero zote zitatuliwe, na niishukuru serikali kwa kumaliza hii kero ya umeme iliyudumu kwa muda mrefu.” Alisema Mhe. Bungara
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(kushoto), akifurahia jambo na Wazitri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, (watatu kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua, (wane kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO), Dkt. Alexander Kyaruzi, na Mkuriugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, wakati alipowasili kuzindua mradi wa upanuzi wa Kituo cha Kufua umeme wa Gesi asilia (Mtwara Gas Plant), mkoani Mtwara Alasiri ya Mei 21, 2018. Kituo hizo sasa kitazalisha Megawati 22 kutoka za sasa Megawati 18.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akitoka eneo la mitambo mipya miwili ya kuzalisha umeme wa Megawati 4 kila mmoja baada ya kuizindua, kwenye Kituo cha Kufua umeme wa Gesi Mkoani Mtwara Mei 21, 2018.
Wabunge wa Mikoa ya Kusini, wakiwa na mwenyekiti wao, Mhe. Selemani Bungara(wapili kushoto) 
Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini, Mhe. Selemani Bungara, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa upanuzi wa Kituo cha Kufua umeme wa Gesi mkoani Mtwara Mei 21, 2018.
Mbunge wa Mtwara Mjini Mhe.Maftah Nachuma, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa upanuzi wa Kituo cha Kufua umeme wa Gesi mkoani Mtwara Mei 21, 2018.
Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...