Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JUMLA ya Wanafunzi 78 kutoka baadhi ya shule za msingi, sekondari na Vyuo Vikuu nchini wametunukiwa Tuzo ya Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke baada ya kuhitimu mafunzo ya lugha ya Kichina huku Wizara ya Elimu ,Sayansi, Teknolojia na Ufundi ikihimiza Watanzania kuchangamkia fursa kwa kujifunza lugha hiyo.

Mafunzo hayo ya lugha ya Kichina na mchakato wa utoaji tuzo hiyo ya Balozi wa China nchini yameandaliwa na Chama cha Kukuza Uhusiano wa China na Tanzania(Tanzania China friendship Promotion Association) ambacho Mwenyekiti wake ni Dk.Salim Ahmed Salim na Katibu Mkuu ni Joseph Kahama.

Akizungumza Dar es Salaam leo kwa niaba ya Waziri wa Elimu ,Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wakati wa utoaji tuzo hizo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk.Ave Maria Semakafu amesema kuhitimu kwa vijana hao 78 kwa kuifahamu lugha ya Kichina kutatoa fursa nyingi kwao ikiwamo ya kupata ajira katika nchi ya China kwani kuifahamu lugha yao ni sawa na kufahamu utamaduni wao.

Amefafanua kwa vijana wa Kitanzania ambao watakuwa wanakifamu vema Kichina ni rahisi kufundisha nchini China na kufanya kazi za aina mbalimbali pale watakapohitaji na kwa Tanzania kuna Shule 24 zinafundisha Kichina na wanafunzi wanaosoma somo hilo wanafanya mtihani.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Dk.Ave Maria Semakafu(aliyevaa gauni)akimkabidhi tuzo ya Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke mwanafunzi  wa Shule ya Nsingi Msoga Arafa Shaibu ambaye amehitimu lugha ya Kichina

 Mgeni rasmi katika utoaji wa Tuzo ya Balozi wa China nchini Tanzania Wang  ambao wamehitimu mafunzo ya lugha ya Kichina,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Dk.Ave Maria Semakafu (wa kwanza mstari wa mbele)akifuatilia hotuba wakati wa utoaji Tuzo hizo
Political Counceller wa Ubalozi wa China nchini Tanzania Yang Tong akizungumza kwa niaba ya Balozi wa nchi hiyo nchini Wang Ke wakati wa utoaji Tuzo kwa wanafunzi 78 wa Tanzania ambao wamehitimu mafunzo ya lugha ya  Kichina.Tuzo hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia utoaji Tuzo ya Balozi wa China nchini Tanzania kwa wanafunzi ambao wamehitimu mafunzo ya Lugha ya Kichina
 Political Conceller wa Ubalozi wa China nchini Tanzania Yang Tong (kushoto)akiwa ameshika tuzo pamoja na mwanafunzi baada ya kumkabidhi
 Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Bao Bao Mariam Said akiwa ameshika tuzo ya Balozi wa China nchini Tanzania baada ya kutunukiwa jijini Dar es Salaam kutokana na kuhitimu mafunzo ya lugha ya Kichina ambayo yameandaliwa na Chama cha Kukuza Uhusiano Tanzania na China
 Baadhi ya raia wa China nchini Tanzania wakiwa wamebeba baadhi tuzo ambazo wametunukiwa wanafunzi waliohitimu kujifunza somo la Kichina.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...