NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeutaka uongozi wa Kambi ya Wazee na watu wasiojiweza Nunge kuwakamata wahusika wanaouza viwanja katika eneo la kambi hiyo .

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akijibu kero za Wazee wa Nunge alipotembelea kambi hiyo iliyopo Kigamboni jijini Dar es salaam.

Sambamba na hilo Dkt. Ndugulile alisimamisha ujenzi wa nyumba ya mwananchi wan je na kambi hiyo uliokuwa unaendelea katika eneo hilo ambalo inadaiwa sio muhusika wa eneo la kambi ya wazee ya Nunge na kusema aliyeuziwa katika eneo hilo Serikali haitamtambua. “Marufuku kwa mtu yeyote kuuza,kununua wala kujenga pamoja na kuchimba mchanga katika eneo la kambi hii na mtu atakayebainika anajihusisha na vitendo hivyo basi hatua za sharia zitafuata zidi yake “ alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa misaada inayokuja katika kambi hiyo iwe inawekwa kwenye utaratibu maalumu ili kila mmoja aweze kupata mahitaji anayostahili kwa wakati husika na viorodheshwe kwenye daftari la kambi hiyo kama kumbukumbu ili kuondoa changamoto ya kurumbana kuhusu mahitaji kwa wazee hao.

Mbali na hayo Dkt. ametoa muda wa wiki mbili tatizo la usafiri kwa wazee wa kambi hiyo liwe limeshughukulikiwa kwa kutengeneza bajaji iliyotolewa na Serikali kwa manufaa ya Wazee wa kambi hiyo na si vinginevyo.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha kambi ya wazee Nunge Dkt. Dismas Chihwalo wakati akisoma taarifa fupi ya kituo hiko amesema kuwa ili uwepo utaratibu mzuri wa kuhudumia walengwa katika kambi hiyo ni lazima kuwepo na makualiano maalumu kwa kutia saini baina ya wanaoletwa kwa mahitaji maalum na viongozi wa kambi hiyo.

“Serikali inatakiwa kuhakikisha wanaoletwa kwa ajili ya huduma maalum na kwa muda maalum wanatia saini mkataba wa makubaliano ili kuweza kuepusha migogoro ya kutoa huduma katika kambi hiyo kwa wanaostahili” alisema Dkt. Chihwalo.Kambi ya Wazee na wasiojiweza Nunge ilianzishwa mwaka 1936 kwa makusudi ya kuwahudumia Wazee na wasiojiweza pamoja na wenye ukoma ili wasipate shida za mahittaji muhimu na huduma za afya kwa wakati sahihi. 
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua chakula wanachopikiwa wazee wa kambi ya Nunge iliyopo Kigamboni wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma kituoni hapo mapema leo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na moja ya binti wa Mhitaji anaeishi katika kambi hiyo ya Nunge iliyopo Wilaya ya Kigamboni, huku lengo la ziara hiyo likiwa kukagua hali ya utoaji huduma kituoni hapo.
 Baadhi ya Wazee waliojitokeza katika ukumbi wa Kituo cha kulelea Wazee wa Nunge ili kupata fursa ya kuzungumza na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pindi alipofanya ziara kituoni hapo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi wake wa jimbo la Kigamboni Wilayani Kigamboni pindi alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma kituoni hapo mapema leo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya viongozi wa kituo cha kulelea wazee cha Nunge na wazee waliojitokeza kumsikiliza pindi alipofanya ziara kituoni hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...