WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameshiriki kazi za ujenzi wa uwanja mpya wa michezo wilayani Ruangwa kwa kubeba zege na matofali pamoja na wananchi.

Waziri Mkuu ambaye pia ni mbunge wa Ruangwa, ameshiriki zoezi hilo leo (Ijumaa, Mei 25, 2018) kwenye uwanja huo unaojengwa katika kijiji cha Dodoma, kata ya Nachingwea, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.

Akizungumza na wananchi na viongozi waliojitokeza kushiriki zoezi hilo, Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na kazi ya ujenzi inayoendelea hadi sasa na akatumia fursa hiyo kuwashukuru wana-Ruangwa kwa kurejesha moyo wa kufanya kazi kwa kujitolea.

“Ninawashukuru sana wana-Ruangwa kwa sababu mmeanza kufanya kazi za kujitolea, haya matofali ni matokeo ya kazi yenu, hakuna hata mtu mmoja amelipwa kwa kazi hii. Nimeambiwa yanahitajika matofali 60,000 kwa ajili ya kujenga uzio lakini hadi sasa mmeshafyatua 57,000 na zaidi, ninawashukuru sana,” amesema.

“Nimeambiwa madiwani walipiga kambi ya wiki moja hapa, Umoja wa Vijana wa CCM nao walipiga kambi, UWT walikuja kusomba matofali, watumishi wa Halmashauri nao walipiga kambi, hongereni sana kwa kurejesha moyo wa kujitolea miongoni mwa wananchi,” amesema.

Katika zoezi la leo, walijitokeza wananchi wengi wakiwemo wazee, vijana na watoto. Baadhi ya watoto walikuwa wakibeba tofali moja kwa kushirikiana wawili wawili, watatu watatu hadi wanne.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akichimba msingi wa  jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwana wananchi  kwenye eneo la Dodoma katika mji mdogo wa Ruangwa mkoani Lindi, Mei 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua nyasi zilizooteshwa kitalaam wakati alipshiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwa kwenye eneo la Dodoma katika mai mdogo wa Ruangwa, Mei 25, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubeba tofali, Bibi Mariam Bakari wakati aliposhiriki katika ujenzi wa  wa msingi wa uwanaja wa michezo unaojengwa na wananchi kwenye eneo la Dodoma katika mji mdogo wa Rungwa mkoani Lindi, Mei 25, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na wanne kushoto ni  Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masala. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubeba tofari Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masala wakati aliposhiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwa na wananchi  katika eneo la Dodoma kwenye  mji mdogo wa Ruangwa,Mei 25, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi  Bi. Khadija Madoa ambaye ni Mama lishe anayeuza chakula katika mji mdogo wa Ruangwa mkopo usiokuwa na riba wa sh. 200, 000/=  baada ya kushiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo wa unaojengwana wananchi katika eneo la Dodoma, Ruangwa mkoani Lindi Mei 25, 2018. Jumla ya sh. milioni 9 zilitolewa na mfanyabiashara Abdallah Mang'onyola na kutolewa mkopo kwa Mama lishe 42.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwa kwenye eneo la Dodoma katika mji mdogo wa Ruangwa mkaoani Lindi Mei 25, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Zahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa, Mei 25, 2018. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...