WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka waumini wa dini ya Kiislamu wajiepushe na vitendo vinavyoweza kupandikiza chuki dhidi yao au kwa waumini wa dini nyingine.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Mei 26, 2018) wakati akizungumza na viongozi na mamia ya waumini wa dini ya Kiislamu walioshiriki mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Quran tukufu kwenye ukumbi wa Mwl. J. K. Nyerere jijini Dar es Salaam.Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Istiqaama Tanzania (Istiqaama Muslim Community of Tanzania), yalijumuisha washiriki 29 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.

“Serikali inatambua na inathamini sana, mchango wa dini katika kuwalea waumini kiimani na kutunza amani ya nchi. Hivyo, tujiepushe na kauli au vitendo ambavyo vinaweza kupandikiza chuki na uhasama dhidi yetu au dhidi ya waumini wa imani nyingine,” amesema.

“Nitoe rai kwenu viongozi wangu na waumini wenzangu, tujenge misingi ya kuvumiliana na kustahamiliana. Hilo pekee ndilo linaloisimamisha nchi yetu kuwa ni mfano wa kuigwa na kimbilio la wale waliovurugikiwa na amani katika nchi zao. Kadhalika, amani inajenga na kutoa fursa ya kuweza kutekeleza majukumu yetu ya kiibada, kiuchumi na kijamii bila hofu,” amesema.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Kombo Faki Hamadi kutoka Pemba zawadi ya Shilingi milioni 4 baada ya kuibuka kuwa mshindi wa kwanza wa Juzuu 30 katika Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu yaliyofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 26, 2018. Katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania (Istiqaama Muslim Community of Tanzania), Seif Ali Seif.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Quraan Tukufu yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania, Mei 26, 2018.
Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir akizungumza katika Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 26, 2018.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania kwenye Kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam,Mei 26, 2018.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania ( Istiqaama Muslim Community of Tanzania), Seif Ali Seif katika Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam,Mei 26, 2018.





Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 26, 2018.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na baadhi ya viongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam waliohudhuria katika Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam,Mei 26, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...