Kiongozi wa HDIF, Tanzania,David McGinty  akizungumza na Wahariri  na Waandishi wa Vyombo Mbalimbali vya habari pamoja na wadau wa Masuala ya Sayansi wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Ubunifu kwa Vijana inayofanyika katika Kumbi Mbalimbali za Costech Jijini Dar es Salaam chini ya ufadhili wa UKAID na HDIF.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),Dkt Amos Nungu akizungumzia kuhusu wiki ya Ubunifu kwa Vijana iliyoanza katika Kumbi mbali mbali za Costech, ambapo wanufaika wataonesha kazi zao kwa kuwasilisha katika makongamano yatakayokuwa yanaendelea  chini ya ufadhili wa HDIF kwa kushirikiana na UKAID
Naibu Kiongozi wa HDIF Tanzania, Joseph Manirakiza akieleza namna HDIF ilivyoweza kutoa ruzuku kwa wanufaika wa miradi mbalimbali ya ubunifu wakati wa ufunguzi ya wiki ya ubunifu inayoendelea katika kumbi mbalimbali za COSTECH.
Baadhi ya wanufaika wa Mradi huo wakifuatilia kwa ukaribu hotuba mbalimbali zinazotolewa na wadau wa masuala ya ubunifu.
Mtaalamu wa Masuala ya Mawasiliano kutoka HDIF , Hannah Mwandoloma akiwa pamoja na baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari wakisikiliza mawasilisho juu ya wiki ya Ubunifu.
Wanufaika wa Wiki ya Ubunifu wakiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa COSTECH, HDIF na UKAID


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...