JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
                                                                                            
  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepata kibali cha Ajira kwa sekta ya afya nchini cha kuwaajiri wataalam wa kada mbalimbali za Afya wapatao 8,000.

Hayo ya mesemwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.

Dkt. Mpoki amesema wamepata kibali hicho kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kuongeza kwamba Wizara yake inalo jukumu la kuwapangia vituo vya kazi waombaji wenye sifa kwa mujibu wa waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Umma Namba 1 wa mwaka 2009 kuhusu miundo ya utumishi wa kada za afya chini ya Wizara ya Afya.

Aidha, alisema kibali hicho chenye aina mbili za mwajiri ikiwepo nafasi 6,180 ambazo zimeenda Hospitali zilizo katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenye hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati. Nafasi 1,820 zimeenda Hospitali zilizo chini ya Wizara ya Afya, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Wizara zingine na Taasisi za Umma pamoja na Hospitali ya Mlongazila na Benjamini Mkapa.

Alitaja sifa za waombaji wa nafasi hizo kuwa, awe raia wa Tanzania, umri usiozidi miaka 45, asiwe mwajiri wa Serikali au mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali na asiwe ameshawahi kufanya kazi Serikalini na kuacha kazi.Hata hivyo, Dkt. Mpoki amewakumbusha wataalam hasa wale wanaosajiliwa na mabaraza ya kitaaluma kuambatanisha nakala za usajili au leseni ya kufanya kazi ya taaluma husika wakati wa maombi hayo.

Katibu Mkuu ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na kueleza kuwa nafasi hizi 8,000 ni juhudi za Serikali za kupunguza uhaba wa rasilimali watu katika sekta ya afya. 

Imetolewa na : 
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya 
11/5/2018

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Samahan nilikuwa mauliza tuna tuma wap hayo maombi yetu

    ReplyDelete
  2. Maombi tunayatuma wap tusaidien

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...