THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WIZARA YA AFYA YATAMBUA UMUHIMU WA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI (GCLA) KULINDA AFYA ZA WANANCHI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MGANGA  Mkuu wa  Serikali  Profesa  Mohamed Kambi amesema Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inatambua umuhimu wa Mamlaka ya Maabara ya  Serikali Mkemia Mkuu katika kulinda ya afya ya wananchi.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto ambapo amesema kikao cha baraza  ni kuhakikisha kuna kuwepo kwa uhusiano kati ya watendaji na Menejimenti.

Kambi amesema katika mkutano wa baraza wanatakiwa kujadili malengo ya taasisi na maslahi ya wafanyakazi ikiwemo mafunzo  ambayo yanatakiwa kutolewa kwa haki sawa.

Aidha Mganga Mkuu huyo ametaka wafanyakazi  wa (GCLA) kuachana na kuwa sehemu ya watu wanaolalamika badala yake wanatakiwa kutatua changamoto zinazowakabili.Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi (GCLA), Dk. Fidelice  Mafumiko  amesema katika kikao  hicho watajadili mada mbalimbali ikiwa ni kuijenga  taasisi hiyo.

Dk. Mafumiko amesema pia baraza hilo kupitia kikao hicho wataazimia mambo mbalimbali yakiwamo ya kujenga mamlaka  ikiwa pamoja na masuala ya maadili.
 Mganga Mkuu wa Serikali,  Profesa Mohamed Kambi  akizungumza katika mkutano wa baraza la  wafanyakazi wa Mamlaka ya Maabara ya  Serikali Mkemia Mkuu (GCLA) uliofanyika katika ukumbi wa MSD  jijini Dar es Salaam .
 Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Maabara ya  Serikali Mkemia Mkuu (GCLA), Dk. Fidelice Mafumiko akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa GCLA  kuhusiana na mada ambazo watapitia uliofanyika katika ukumbi wa MSD jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Tawi la la TUGHE wa GCLA, Juvitus Mukela akitoa neno kwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa GCLA uliofanyika katika ukumbi wa msd jijini Dar es Salaam .
 Baadhi ya wajumbe katika mkutano wa baraza la wafanyakazi wa GCLA wakifuatilia mada kwenye mkutano huo.
  Picha za pamoja