Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika Yanga wameshindwa kuondoka na ushindi dhidi ya Rayon ya Rwanda baada ya kulazimishwa suluhu ya kutokufungana.

Yanga waliokuwa katika dimbani la nyumbani la Uwanja wa Taifa walikubali matokeo hayo baada ya kushindwa kupata goli la ushindi ma matokeo kuishia 1-1.

Mchezo huo ulioanza majira ya saa 1 usiku Yanga waliweza kucheza vizuri katika kipindi cha kwanza wakionekana kutawala sehemu ya kiungo kilichokuwa kinaendeshwa na Thaban Kamosoku na Pius Buswita.
Kocha msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amesema kuwa hajaridhishwa na matokeo ya leo dhidi ya Rayon Sports kwani walihitaji ushindi ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwenda hatua inayofuata.

"Sijaridhishwa na matokeo ya leo, katika mchezo huu tulihitaji ushindi ili kuweza kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda hatua inayofuata ila wachezaji walikosa umakini na kushindwa kutumia nafasi walizozitumia,"amesema Mwandila.

Mwandila amesema kwa sasa mashindano haya yanasimama kwa muda mpaka mwezi wa saba kwahiyo watatumia kipindi hiki kwa ajili ya kukiunda kikosi na kukifanyia marekebisho kwenye nafasi zinazohitajika na zaidi watahakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo inayofuata.
Baada ya mechi hii Yanga wanakuwa na alama 1 baada ya mchezo wa kwanza kufungwa huku Rayon wakiwa ma alama 2.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...