Na Anthony Ishengoma WAMJW.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa unaonesha kuwa kati ya asilimia 7 na 16 ya wanawake wote duniani ni Wajane.
Jamii imetakiwa kuendeleza mipango na kuongeza juhudi zaidi katika kukabiliana na vitendo vya ukatili, unyanyasaji na kuwainua wajane ili wapate uwezo wa kiuchumi wa kuzihudumia familia na wategemezi wao kwa kuwa ndiyo muhimili pekee wa familia iliyoachwa.
Akiongea kwa niaba ya Mgeni rasmi wa kongamano la Wajane liliofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa Bi. Honoratha Rwegasira amepongeza juhudi za wadau wa maendeleo na serikali katika kuwasaidia wajane kuleta usawa wa kinjisia na kuinua ushiriki wao katika ngazi za kutoa maamuzi.
Aidha Bi.Rwegasira ameitaka jamii kuacha mila potofu kama vile kunyanganya mali mjane, kuozesha watoto wa kike katika umri mdogo, kurithi wajane na nyingine zote zinazoweza kumdhoofisha mwanamke katika jitihada zake za kujikwamua kifikra, kiutamaduni, kiuchumi,kijamii na kisiasa.
Mkurugezi
Msaidizi Idara ya Jinsia, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Bi. Mwajuma Magwiza akitoa hutuba yake kwenye Kongomano
la Wajane lililofanyika leo Mjini Dodoma.
Afisa
Mwandamizi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Bi .Sirivia Siliwa akitoa mada kuhusu Chimbuko la Siku ya Wajane
Duniani wakati wa Kongomano la Wajane lilifanyika leo Mjini Dodoma.
Mwakilishi
wa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bi. Honoratha Rwegasira akitoa hutuba
ufunguzi kwa niahaba ya Mgeni rasmi wakati wa Kongomano la Wajane
lililofanyika leo Mjini Dodoma.
Wajane
wa Mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye Kongomano la Wajane lililofanyika leo
Mjini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...