Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Benki ya I&M imeandaa futari Maalum kwa ajili ya wateja wake wa Dar es Salaam katika kuadhimisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza wakati wa futari hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki I&M Baseer Mohamed amesema kuwa anawashukuru wateja wa benki hiyo kwa kuendelea kuwapa ushirikiano wa kibiashara ambao umeifanya benki hiyo kuendelea kusimama vyema.

“Mwezi wa Ramadhani unajulikana kama moja ya nguzo za Dini ya Kislamu na Benki ya I&M kwa kutambua umuhimu wake katika Jamii imeandaa futari hii kama sehemu ya matendo yanayopaswa kufanywa na wanajamii katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani” Amesema Baseer

Baseer amesema kuwa benki itaendelea kutekeleza mkakati wake wa kibishara wa mwaka 2018 na kuhakikisha kuwa inaendelea kupata ukuaji ni endelevu na kutaja kuwa wamejipanga kuanzisha huduma mpya ya pamoja na kutanua wigo wetu wa utoaji huduma kupitia njia mbadala za utoaji wa huduma za kibenki. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki I&M Baseer Mohamed akizungumza na Wateja wa benki hiyo waliofika katika futari iliyoandaliwa na Benki yake katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Mkurugenzi wa bodi ya Benki I&M,Alan Mchaki akitoa neno la Shukrani kwa wateja waliofika katika futari hiyo
Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja Ndabu Swere akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya huduma za benki hiyo katika kipindi cha mwaka 2018.
Sehemu ya Wateja wa Benki ya I&M Wakifuatilia hotuba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo
Wateja wa Benki I& M wakipakua futari mara baada ya swala katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Wateja wa Benki I& M wakipakua futari mara baada ya swala katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Sehemu ya Wafanyakazi wa Benki I& M wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya futari katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam-

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...