KUFIKIA 14 Juni, 2018 benki ya Exim Tanzania ilifikia kilele cha kampeni inayoenda kwa jina la "Kupata damu katika benki ya damu kesho, leo" ambayo imejikita kuwahamasisha wananchi kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu inayofanyika kila tarehe 14 Juni duniani kote.

Lengo kuu la kampeni hiyo ambayo iliendana sambamba na kauli mbiu ya benki hiyo inayosema “Exim kazini leo kwa ajili ya kesho” ni kuchangisha damu na kutoa elimu ya umuhimu wa kuchangia damu katika mpango wa taifa. Kampeni hiyo inaonyesha kuwa benki ya Exim iko makini kutafuta njia za ubunifu za kuhudumia wateja wake na muhimu zaidi, inajitolea kuhakikisha inashirki kuleta mabadiliko chanya katika jamii. 

Mpango huu kila mwaka unalenga kukusanya damu kwa ajili ya benki ya taifa chini ya usimamizi wa Mpango wa Taifa wa uchangiaji damu nchini [NBTS]. 

Kampeni hii ilianza rasmi katika tawi la Exim mkoani Arusha tarehe 4 Juni na kuendelea katika mikoa ya Mbeya, Dodoma na Mwanza. Tukio kuu limefanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyakazi 200 , wateja na jamii chini ya kauli mbiu ya kimataifa: " “Jitoe kwa ajili ya mwingine. 

Changia damu." Kampeni hii inakumbusha jukumu la kila mtu kujitolea katika kuwasaidia wengine katika hali ya dharura kwa kutoa zawadi ya thamani ya damu. Pia inasisitiza juu ya ukweli kwamba ni muhimu kutoa damu mara kwa mara ili kuhakikisha kuwepo na damu ya kutosha kabla ya dharura kujitokeza. Kampeni hii ni sehemu ya programu ya majukumu ya shirika la kijamii ya benki ya Exim Tanzania iitwayo, Exim Cares. 
Afisa uhamasishaji wa mpango wa taifa wa Damu salama, Mariam Juma akimpima damu mfanyakazi wa Exim Bank Daniel Lukuba wakati wa kampeni ya uhamasishaji watu kuchangia damu kwa hiari kwa kushirikiana na Damu Salama iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo, posta mjini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya watoaji damu duniania (World Blood Donors Day 2018). 
Afisa Muuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama akimtoa damu mfanyakazi wa Exim Bank Patrick Masawe wakati wa kampeni ya uhamasishaji watu kuchangia damu kwa hiari kwa kushirikiana na Damu Salama iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo, posta mjini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya watoaji damu duniani (World Blood Donors Day 2018). 
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim waitoa damu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...