MAMLAKA ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA) imewaasa watendaji katika masoko ya  Mitaji kuhudhuria mafunzo yanayotambulika katika viwango vya kimaitafa ili kupata ujuzi na kuwa wabobezi katika masoko ya kimaitafa.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama, katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya Watendaji katika Masoko ya Mitaji (SICC) iliyoendeshwa kati ya CMSA na Taasisi ya Uwekezaji na Dhamana (CISI) ya nchini Uingereza.

Alisema chini ya kifungu namba 32 cha Sheria ya Masoko ya Mitaji ya 1994 kama ilivyorekebishwa mwaka 2010, mtu yeyote anayetaka kutoa huduma katika masoko ya mitaji kama Dalali wa Soko la Hisa, Mwakilishi wa Dalali wa Soko la Hisa, Mshauri wa Uwekezaji, Mwakilishi wa Mshauri wa Uwekezaji, Mshauri Mteule, Mwakilishi wa Mshauri Mteule au mtendaji yeyote katika masoko ya mitaji ni lazima apitie mafunzo yanayotolewa na CMSA na kufaulu.

Mkama alisema lengo la sharti hilo ni kuhakikisha kuwa watendaji na wataalamu katika masoko ya mitaji wanakuwa na ujuzi stahiki katika utoaji wa huduma za masoko ya mitaji ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri katika uuzwaji wa dhamana kwa umma na uorodheshwaji wake kwenye masoko ya hisa. "Tangu kuanzishwa kwake, CMSA imekuwa ikitoa mafunzo hayo na mpaka sasa zaidi ya watalamu 560 wamefuzu," alisema. 

Alisema katika utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Afrika Mashariki, (East African Common Market Protocol), Taasisi za Usimamizi wa Masoko ya Mitaji za Afrika (EASRA) zilipitisha na kukubaliana kuwa watendaji wanaotaka kutoa huduma katika masoko ya mitaji ya Afrika Mashariki ni lazima wapitie mafunzo na kufaulu mtihani unaotambulika kimataifa.
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama, akizungumza katika mafunzo ya  watendaji  katika masoko ya mitaji ikiwa ni utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kisera, kisheria na kiutendaji unaofanywa na CMSA.
Meneja Mahusiano wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), Charles Shirima, akizungumza katika mafunzo ya  watendaji katika masoko ya mitaji ikiwa ni utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kisera, kisheria na kiutendaji unaofanywa na CMSA.
Meneja Mahusiano wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), Charles Shirima, akizungumza katika mafunzo ya  watendaji katika masoko ya mitaji ikiwa ni utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kisera, kisheria na kiutendaji unaofanywa na CMSA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...